Naibu Mhasibu Mkuu wa Serikali
wamesimamishwa kazi kutokana na upotevu
mkubwa wa fedha.
Akizungumza na waandishi wa habari visiwani
Zanzibar jana, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk.
Khalid Salum Mohamed, alisema kati ya watendaji
hao wamo wahasibu wakuu wa wizara sita
wanaohusika na upotevu huo wa fedha.
“Kwa masikitiko makubwa naomba kutoa taarifa
kuwa tumebaini upotevu wa fedha za serikali
ambao tumeanza kuuchukulia hatua,” alisema
waziri huyo.
Alisema upotevu huo wa fedha unaonekana sio
wa bahati mbaya, bali ni jambo la kupangwa na
umetekelezwa kwa njama za watendaji wa vitengo
vya fedha uliowahusisha wahasibu.
Aidha, alisema hadi sasa kuna hundi zenye
thamani ya Sh. milioni 571 zimeshindwa kulipwa
kwa sababu ya uhalifu huo na hatua za awali za
kutathmini upotevu huo zinaonyesha kuwa kiasi
ambacho kinahusika na wizi huo kinaweza kuwa
kikubwa zaidi ya hicho.
“Tulipopata taarifa za awali juu ya upotevu huu
hatua za haraka zilichukuliwa na kubaini
wahusika wakuu” alisema Dk. Khalid.
Alisema taarifa za awali zinaonyesha upotevu huo
wa fedha umetokana na njama za baadhi ya
watendaji wa kitengo cha malipo katika Wizara ya
Fedha na Mipango wakishirikiana na baadhi ya
wahasibu wa wizara tofauti za serikali.
Waziri huyo alisema hatua hiyo imezingatia
matakwa ya Sheria ya Fedha za Umma namba 12
ya mwaka 2005 na kanuni zake na Sheria ya
Utumishi wa Umma ya mwaka 2014 na kanuni
zake.
Alisema kutokana na ukubwa wa upotevu huo wa
fedha, hatua itakayofuata ni kuundwa kwa bodi ya
uchunguzi ambayo itakuwa na watu wanne
watakaoteuliwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya
Fedha na Mipango.
Alisema azma ya serikali ni kuimarisha utawala
bora na kuimarisha usimamizi wa fedha za
umma, hivyo watendaji wote wanapaswa
kufahamu kuwa azma hiyo inatekelezwa bila ya
kuyumba wala kumuonea haya mtu yeyote.
Chapisha Maoni