Khatib, ameitaka serikali kukifutia usajili Chama
cha Wananchi (CUF), kwa madai kuwa kimekuwa
kikishiriki katika matukio ya kupigwa na kuharibu
mali za wananchi visiwani Pemba.
Mbunge huyo alitoa kauli hiyo jana, alipokuwa
akiuliza swali la nyongeza katika kipindi cha
maswali na majibu bungeni.
“Kutokana na kuwapo matukio ya wananchi
kupigwa hususan wanachama wa CCM, ni kwanini
serikali isikifutie usajili chama cha CUF kwakuwa
ndio chanzo cha matukio hayo visiwani
pemba,” alihoji Mbunge huyo.
Katika swali la Msingi la Mbunge wa Chambani
(CUF), Yusufu Salim Hussein, naye alihoji kama
serikali inatambua tatizo la raia kupigwa na
kuharibiwa mali zao kwa upande wa Zanzibar,
ambalo limekuwa likiongezeka siku hadi siku na
hatua gani zimechukuliwa.
Kutokana na masuala hayo, wabunge walionekana
wakisimama kuuliza maswali ya nyongeza na
Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Tauhida Cassian
Nyimbo, alihoji serikali inachukua hatua gani kwa
viongozi wa CUF ambao wamekuwa wakitoa kauli
za vitisho kupitia mitandao ya kijamii na
kuwafanya wananchi visiwani humo kuwa na hofu
hasa kipindi hichi cha kuelekea sikukuu ya Idd el
Fitri.
Naye Mbunge wa Dimani (CCM), Hafidh Ali Tahir,
alihoji ni kwa namna gani serikali
itawashughulikia baadhi ya viongozi ambao
wamekuwa na tabia ya kuvunja sheria na
maagizo ya viongozi kuhusu mikutano ya
hadhara.
Akijibu maswali hayo, Naibu Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Hamad Yusuf Masauni, alisema
serikali inatambua kwamba kila unapofika wakati
wa Uchaguzi Mkuu hasa katika kisiwa cha Pemba,
baadhi ya watu hujichukulia sheria mkononi kwa
kuwapiga wengine na kuharibu mali zao.
Kutokana na hali hiyo, alisema serikali itaendelea
kuongeza vikosi vya ulinzi na usalama katika
maeneo yote tete na kuhakikisha utii wa sheria
bila shuruti unazingatiwa.
“Pia serikali itaendelea kuwaelimisha wananchi
madhara ya kujichukulia sheria mikononi dhidi ya
wengine wasio na hatia,” alisema Masauni.
Alitoa wito kwa wananchi wote kuacha mihemko
ya itikadi za kisiasa wakati na kabla ya uchaguzi
kwani hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi
yao.
Kuhusu viongozi wanaokiuka maagizo ya serikali
kuhusu mikutano ya kisiasa, Masauni alisisitiza
mikutano hiyo haitakiwi kwa wakati huu hadi
hapo polisi itakapoona inafaa na kuvitaka vyama
vya siasa kutii maagizo ya serikali.
“Hakuna mtu ambaye yuko juu ya sharia. Wale
watakaoleta ukorofi watachukuliwa hatua kali bila
kujali kama ni kiongozi wa aina gani na mahali
gani anatokea. Lazima sheria ichukue mkondo
wake,” alisema.
Kuhusu suala la kukifuta CUF, Naibu Waziri huyo
alisema jukumu hilo si la serikali bali limo
mikononi mwa Msajili wa vyama vya siasa,
ambaye anatakiwa kuliangalia kwa mujibu wa
sheria na taratibu zilizopo.
Aidha, alisema nchi iko salama na serikali
itaendelea kuhakikisha amani na utulivu
vinakuwapo wakati wa sikukuu hiyo na kuwataka
wananchi kupuuza kauli za uchochezi
zinazotolewa na wanasiasa.
Baada ya kipindi hicho, Mbunge wa Mwibara,
(CCM), Kangi Lugola, aliomba mwongozo kwa
Naibu Spika akisema ni kwa nini serikali ipo
bungeni; isitoe majibu kuhusiana na matukio
yanayofanywa na CUF ambayo mbunge
mwenzake amependekeza kifutiwe usajili na
badala yake inatoa jukumu kwa msajili wa vyama
vya siasa wakati ni sehemu ya serikali.
Kutokana na mwongozo huo, Naibu Spika wa
Bunge, Dk. Tulia Ackson, alisema atatoa majibu
ya mwongozo huo baada ya kupitia sheria ya
vyama vya siasa inasemaje.
Chapisha Maoni