Visiwani kuwa nchi iko salama na inaendelea
kuwa salama pamoja na kuwapo kwa vitisho kwa
njia ya mtandao.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Naibu Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yussuf
Masauni, wakati wa kujibu swali la nyongeza la
Mbunge wa Viti Maalumu, Tauhida Nyimbo (CCM)
aliyetaka kauli ya serikali kutokana kuwapo kwa
taarifa za vitisho zinazotolewa kwenye mtandao
wakati huu wa maandalizi ya sikukuu ya Idd el
Fitr.
Alisema pamoja na kuwapo kwa vitendo vya
kiuhalifu vinavyotokea, nchi bado iko salama na
itaendelea kuwa salama kutokana na serikali
kuhakikisha inadhibiti uhalifu huo.
Serikali imeendelea kusisitiza kuwa mikutano ya
kisiasa itaendelea kuzuiwa hadi pale polisi
watakapoona inafaa kufanyika.
Chapisha Maoni