wameondoshwa katika michuano ya Euro 2016
baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka
kwa Italia.
Italia iliweza kuibana vyema Hispania kipindi chote
cha kwanza na ilifanikiwa kupata bao la kuongoza
kupitia kwa Giorgio Chiellini aliyemalizia mpira wa
adhabu uliokuwa umetemwa na kipa wa Hispania
David De Gea.
Kipindi cha pili Hispania ilirudi kwa nguvu ikisaka
bao la kusawazisha, iliweza kutengeneza nafasi
kadhaa za kufunga lakini ilikwamishwa na uimara
wa mlinda lango wa Italia, Buffon.
Italia ilipata bao la pili kwenye dakika za majeruhi
baada ya kufanya shambulizi la kushitukiza, pasi
ya Matheo Damian ilimaliziwa vyema na Pelle.
Sasa Italia itakumbana na Ujerumani kwenye hatua
ya robo fainali ya michuano hiyo.
Island nayo imeweza kutinga hatua ya robo fainali
baada ya kuilaza Uingereza mabao 2-1.
Kisiwa hicho chenye wakazi chini ya laki tatu
kimeweza kuishangaza dunia kwa kuwarudisha
nyumbani waingereza mapema kabisa.
Isaland ilitokea nyuma kupachika mabao yake
baada ya kufungwa mapema ambapo Uingereza
kupitia kwa Wayne Roone iliandika bao kwenye
dakika ya tatu baada ya Raheem Sterling kufanyiwa
madhambi ndani ya 18 hivyo mwamuzi kuamuru
ipigwe penati.
Hata hivyo dakika mbili baadae Island ilisawazisha
bao hilo kupitia kwa Sigurdsson baada ya
Waingereza kuzembea kuondosha mpira wa hatari
langoni mwao.
Sigthorsson aliifungia Island bao la pili kwenye
dakika ya 18 baada ya kuwazidi ujanja walinzi
watatu wa Uingereza na kufanikiwa kupiga mpira
uliomparaza kipa namba moja wa Uingereza Joe
Hart na kutinga wavuni.
Licha ya kufanya kila namna kujaribu kusawazisha,
jahazi la Waingereza lilizama mikononi mwa
Island.
Island sasa inakwenda kupambana na Ufaransa
kwenye hatua ya robo fainali July 03.
Aidha baada ya kipigo hicho, kocha wa Uingereza,
Roy Hodgson alitangaza kujiuzulu nafasi yake.
Hodgson amesema kipigo hicho kimemsononesha
hivyo hana budi kuachia ngazi kumpisha mtu
mwingine atakaiongoza timu hiyo.
Juni 30, mchezo wa kwanza wa robo fainali
utazikutanisha Poland na Ureno, July mosi Wales
itachuana na Belgium wakati July pili Italia
itaumana na Ujerumani.
Chapisha Maoni