Msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji mstaafu
Francis Mutungi amewataka wanasiasa kutoitafisri
vibaya hotuba ya Rais kwamba amepiga marufuku
shuguli za kisiasa na badala yake watambue kuwa
alichosema Rais ni kwamba amefungua milango ya
mashirikiano na wanasiasa katika kuendeleza Taifa
kwa kufanya kazi na siyo muda wote kuhubiri
siasa.
Kiongozi huyo ameyasema hapo Jijini Dar es
Salaam wakati wa maadhimisho ya wiki ya
utumishi wa umma ambapo alitoa maoni hayo
kama mmoja ya wadau wa siasa za Tanzania na
kusema kuwa inashangaza kuona kuwa baadhi ya
watu wamechukua kipande kidogo cha hotuba ya
Rais na kukitolea tafsiri ambazo wao wanaona ni
kizuri kwao na kupotosha maana nzima
iliyokusudiwa.
Aidha kiongozi huyo amevitaka vyama vya siasa
nchini kuhakisha vinafuta sheria na taratibu
zilizotungwa katika kuendesha vyama vyao
ikiwenmo kuwasilisha taarifa za gharama za
uchaguzi kama sheria inavyoelekeza.
ITV
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni