0
KOCHA wa timu ya taifa ya
vijana ya Nigeria chini ya
umri wa miaka ya 23,
Samson Siasia amemuita
Nahodha wa Super Eagles,
John Mikel Obi (pichani
kushoto) katika kikosi cha
awali cha wachezaji 34 kwa
kambi ya kujiandaa na
michezo ya Olimpiki nchini
Marekani.
Kikosi hicho kitapunguzwa
na kubaki na wachezaji 18
ambacho kitasafiri kwenda
mjini Rio de Janeiro, Brazil
baadaye mwaka huu kwenye
michezo hiyo.
Shirikisho la Soka Nigeria
(NFF) limesema kikosi cha
Olimpiki kitaondoka wiki
ijayo kwenda kwenye kambi
ya maandalizi Marekani.
NFF imethibitisha kutakuwa
na mchezo wa kirafiki ya
kujipima nguvu dhidi ya
Mexico nchini Mexico
Jumamosi ya Julai 2, mwaka
huu Uwanja
wa Aguascalientes, ambao
unamilikiwa na klabu ya
Necaxa FC iliyopanda Ligi
Kuu ya nchi hiyo.
NFF imesema baada ya
mchezo huo, U23 ya Nigeria
itaendelea na kambi yake
nchini Marekani na itacheza
na Charleston Battery FC
mjini Atlanta Jumamosi ya
Julai 16, wakati pia kuna
mpango wa kucheza na U23
ya Honduras Julai 27.
Kikosi kamili cha awali cha
Nigeria kwa ajili ya Olimpiki
kinaundwa na Daniel Akpeyi
(Chippa FC, Afrika Kusini),
Yusuf Bala (Kano Pillars),
Emmanuel Daniel (Enugu
Rangers), Taiwo
Abdulrahman (Kwara United),
Ndubuisi Agu (FC Porto,
Ureno), Junior Ajayi (CS
Sfaxien, Tunisia), Stanley
Amuzie (Olhanense FC,
Ureno), Taiwo Awoniyi
(Frankfurt FC, Ujerumani),
Okechukwu Azubuike (Yeni
Malatyaspor, Uturuki), Etor
Daniel (Enyimba FC),
Augustine Dimgba (Sunshine
Stars), William Ekong
(Haugesund FC, Norway),
Saturday Erimuya (Kayseri
Erciyespor, Uturuki),
Oghenekaro Etebo (CD
Feirense FC, Ureno), Imoh
Ezekiel (Anderlecht, Belgium),
Saviour Godwin (Ostende,
Ubelgiji), Odion Ighalo
(Watford FC, England),
Kelechi Iheanacho
(Manchester City, England),
Alex Iwobi (Arsenal FC,
England), Emiloju Julius
(MFM FC), Kingsley Madu (AS
Trencin, Slovakia), John
Mikel Obi (Chelsea FC,
England), Musa Muhammed
(Istanbul Basaksehir,
Uturuki), Usman Muhammed
(CF Uniao, Ureno), Wilfred
Ndidi (KRC Genk, Ubelgiji),
Erhun Obanor (MFM FC),
Godfrey Oboabona (Caykur
Rizespor, Uturuki), Kenneth
Omeruo (Chelsea FC,
England), Sodiq Saliu
(Seraing FC, Ubelgiji),
Abdullahi Shehu (CF Uniao,
Ureno), Moses Simon (KAA
Gent, Ubelgiji), Seth Sincere
(Rhapsody FC), Ndifreke Udo
(Abia Warriors), Aminu Umar
(Osmalispor, Uturuki) na
Sadiq Umar (AS Roma, Italia)

Chapisha Maoni

 
Top