0
Mshambuliaji wa Real Madrid James Rodriguez, 24,
ameambiwa anaweza kuondoka Santiago Bernabeu
na kwenda Old Trafford lakini ikiwa tu Manchester
United watatoa pauni milioni 50 (Daily Mirror),
nafasi ya Rodriguez huenda ikazibwa na kiungo
mchezeshaji wa West Ham Dimitri Payet, 29,
ambaye Zinedine Zidane amesema mchezaji huyo
anaweza kuwa mchezaji mzuri katika klabu yoyote
Ulaya (Daily Mirror), meneja mpya wa Manchester
City Pep Guardiola amempigia simu kumpa moyo
mshambuliaji wa England Raheem Sterling, 21,
ambaye amekuwa akisuasua kwenye michuano ya
Euro. Sterling alizomewa na baadhi ya mashabiki
wa England kwenye mchezo dhidi ya Wales, na
hakuchezeshwa kwenye mechi dhidi ya Slovakia
(Guardian), Nolito, 29, anayesakwa na Manchester
City amekiambia kituo cha redio cha Marca kuwa
„kwa sasa sijasaini Man City, lakini sidanganyi,
tusubiri tuone.” City wako tayari kulipa pauni
milioni 13.8 kumsajili mchezaji huyo wa Celta Vigo
(Manchester Evening News), mshambuliaji wa
Everton, Romelu Lukaku, 23, amesema anamuachia
wakala wake kushughulikia mustakabali wake.
Mchezaji huyo amehusishwa na kurejea Chelsea
(Sky Sports), meneja mpya wa Chelsea Antonio
Conte amepewa jukumu la kuirejesha Chelsea
kwenye ‘Top Four’ baada ya klabu hiyo kumaliza
katika nafasi ya 10 msimu uliopita (Daily Mail),
Sunderland, Manchester United, Everton na
Southampton wanamfuatilia mchezaji wa kimataifa
wa Uturuki Ozan Tufan, 21. Mchezaji huyo wa
Fernabahce alifunga goli wakati Uturuki iliposhinda
2-0 dhidi ya Jamhuri ya Czech kwenye michuano
ya Euro (The Chronicle), Watford nao pia
wameanza kumfuatilia winga wa Newcastle, Andros
Twonsend, 24 (Daily Mirror), mshambuliaji wa
Manchester United Ashley Fletcher, 20, amekataa
mkataba mpya wa kubakia Old Trafford. Aliichezea
Burnley kwa mkopo msimu uliopita na huenda
akahamia Leeds United (Yorkshire Evening Post),
mshambuliaji wa Everton Oumar Niasse, 26,
ananyatiwa na Galatasaray (Talksport), Chelsea,
Manchester United na Arsenal wote wanamtaka
mshambuliaji wa kimataifa wa Spain Alvaro Morata,
23. Real Madrid wametumia haki yao ya kumnunua
tena kutoka Juventus mapema wiki hii lakini
wanaweza kumuuza tena (Squawka). 

Chapisha Maoni

 
Top