Arsene Wenger ana kazi ya kuzuia kikosi chake kisimeguke ili kuwa na nguvu ya kupigania mataji msimu ujao baada ya kuwape na vigogo wanaotaka kuvamia kikosi chake.
Wakati Wenger akihaha kutengeneza kikosi makini
cha Arsenal kwa msimu ujao akiwa tayari amemsajili kiungo wa Uswisi, Granit Xhaka, kuna
klabu vigogo vinawafukuzia kimyakimya mastaa wake.
Ripoti zimefichuka kwamba nyota ambao Arsenal
haitapenda kuwapoteza ni Alexis Sanchez, lakini staa huyo anawindwa kwa nguvu zote na vigogo
wa Ulaya ikiwamo Juventus ya Italia.
Juventus, ambayo inaamini kwamba huenda
ikampoteza Paul Pogba katika dirisha la uhamisho
wa majira haya ya kiangazi barani Ulaya,
limemweka Sanchez kuwa kinara katika orodha ya
wachezaji inaotaka kuwasajili mwaka huu.
Juventus wanashawishika na kauli kutoka kwenye
kambi ya Sanchez kwamba, kuhama ni jambo
linalowezekana na kwenye soka lolote linaweza
kutokea muda wowote.
Juventus tayari ina pesa baada ya kufanya
biashara na Real Madrid juu ya mchezaji Alvaro
Morata na sasa wanataka kutumia mshiko huo
kumnasa Sanchez.
Juventus inataka mchezaji ambaye atakuwa na
uwezo wa kuleta ushindani kwenye Ligi ya
Mabingwa Ulaya.
Tayari imeshamsajili Miralem Pjanic kutoka AS
Roma na sasa inamtaka Sanchez kwa nguvu.
Mwanaspoti
Chapisha Maoni