Ivory Coast wamekuwa wakilazimishwa kuhama
makwao baada ya ubalozi wa Marekani kuchapisha
picha yao wakiweka sahihi kwenye kitabu cha
rambi rambi kwa waathiriwa wa mauaji
yaliyofanyika katika klabu moja ya wapenzi wa
jinsia moja mjini Orlando jimbo la Florida nchini
Marekani.
Picha iliyochapishwa kwenye mtandao wa ubalozi
wa Marekani na kusambazwa kwenye mitandao ya
kijamii, ilionyesha wanaume sita wakiweka sahihi
kwenye kitabu cha rambi rambi.
Shirika la habari la AP lilizungumza na wanaume
hao wote wanne ambao hawakutaka kutajwa
majina.
Wawili kati yao wanasema kuwa walishambuliwa
na kundi la watu huku wengine wawili nao
wakisema kuwa shinikizo za kifamilia
zimewalazimu kuhama nyumbani.
Ivory Coast ni moja ya nchi ambazo hazikubali
mahusiano ya jinsia moja.
Chapisha Maoni