0
Sheria za kimataifa hususani kipengele cha 16 cha mkataba wa kimataifa wa kulindwa
kwa haki za Mtoto duniani zinaonekana
kuvunjwa nchini Israel ambako nchi hiyo
inawashikilia mateka Watoto wa
Kipalestina wanaokadiriwa kufikia 438
katika magereza yao.
Habari kutoka katika kituo cha utafiti wa
mateka wa Kipalestina kinadai kuwahivi
karibuni mtoto wa kipalestina Shadi Faraj
mwenye umri wa miaka 12 alifikishwa
kwenye mahakama moja nchini Israel kwa
mara ya tatu na kesi yake kuahirishwa bila
kujulikana hasa kosa la mtoto huyo ni lipi.
Kwa mujibu wa mkuu wa kitengo cha
habari wa kituo hicho Riyadh
Ashqar,amesema katika ripoti yake
aliyoituma kwenda kwa manasaba wa
maadhimisho ya siku ya kimataifa ya
kupambana na mateso (QUDS) kwamba
utwala wa kizayuni wa Israel unatumia
mbinu 80 za mateso ya kimwili na kiroho
dhidi ya mateka wa Kipalestina.
Ripoti ya hivi karibuni ya mfuko wa Watoto
wa U moja wa Mataifa (UNICEF) inaonesha
kuwa utawala wa kizayuni wa Israel ndiyo
utawala pekee duniani unaowapandisha
kizimbani kwa makusudi na kwa lengo
maalumu, watoto wadogo tena kwenye
mahakama za kijeshi.
Siku hii ya kimataifa ya QUDS
huadhimishwa kila mwaka siku ya Ijumaa
ya mwisho ya Mwezi Mtukufu wa
Ramadhani, hii ina maana kesho ndiyo siku
yenyewe.

Chapisha Maoni

 
Top