0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli amesema kwamba wakuu
wa wilaya ambao walikuwa wakifanya kazi hiyo
katika maeneo mbalimbali na kuachwa katika
uteuzi wake maana yake hawakukidhi vigezo
vinavyotakiwa.
Rais Dkt. Magufuli ameyasema hayo alipokuwa
akihutubia wakuu wa wilaya aliowateua hivi
karibuni ambapo wakuu wa wilaya 139 waliteuliwa
huku wengi wakiachwa katika uteuzi huo na nafasi
zao kuzibwa na watu wengine.
Rais Dkt. Magufuli amesema uteuzi huo
umezingatia vigezo vya uwajibikaji na uchapaji
kazi katika maeneo yao, hivyo walioachwa
hawakufanya vizuri inavyotakiwa.
"Wakuu wa wilaya tulioachwa hawakufikia vigezo
tulivyokuwa tunavitaka pia tumechukua
wakurugenzi 22 waliofanya vizuri katika wilaya
zao" - amesema Rais Dkt. Magufuli.
Aidha Rais amewataka wakuu hao wa wilaya
kuchapa kazi na kutumia mamlaka yao vizuri ili
kuweza kutatua kero za wananchi na kuhakikisha
haki ili waweze kumuwakilisha vyema katika nafasi
walizoteuliwa.

Chapisha Maoni

 
Top