0
Mshambuliaji wa Barcelona, Neymar na Douglas Costa wa Bayern Munich wametajwa katika kikosi
cha Brazil kitakachokwenda Rio kwenye michuany ya Olimpiki 2016. Wachezaji hao wenye umri wa zaidi ya miaka 23 ni kati ya watatu tu wanaoruhusiwa kwenda Olimpiki. Mchezaji
mwingine wa umri wa juu ni kipa wa Palmeiras,
Fernando Prass. Gabriel Barbosa, chipukizi wa Santos aliyefunga bao kwenye mechi yake ya
kwanza kwa Brazil mwezi uliopita, ni mmoja kati ya
washambuliaji watano kwenye kikosi hicho cha wachezaji 23. Kocha wa vijana chini ya miaka 20,
Rogerio Micale ndio atakuwa msimamizi wa kikosi hicho baada ya Dunga kufukuzwa kazi kufuatia
kutolewa kwenye Copa America.
Kikosi kamili: Makipa: Fernando Prass (Palmeira),
Uilson (Atletico Mineiro).
Mabeki: Marquinhos (PSG), Luan (Vasco da Gama),
Rodrigo Caio (Sao Paulo), Zeca (Santos), William
(Internacional), Douglas Santos (Atletico Mineiro).
Viungo: Thiago Maia (Santos), Rodrigo Dourado
(Internacional), Fred (Shakhtar Donetsk), Rafinha
(Barcelona), Felipe Anderson (Lazio).
Washambuliaji: Neymar (Barcelona), Douglas Costa
(Bayern Munich), Gabriel Jesus (Palmeiras), Gabriel
Barbosa (Santos), Luan (Gremio).

Chapisha Maoni

 
Top