0
Kesi iliyokuwa inaunguruma kuanzia tarehe
29.02.2016 katika mahakam kuu jijini Arusha
imetolewa hukumu leo hii
Katika shauri hilo aliyekuwa mgombea ubunge wa
CCM jimbo la Longido Dr KIRUSWA alifikisha
mahakamni shauri hilo la kupinga matokeo ya
ushindi dhidi ya mbunge wa Longido mh
ONESMO NANGOLE
Akisoma hukumu hiyo,Jaji MWAGESI alisema
kwamba mlalamikaji ndugu Kiruswa aliwakilishwa
na Wakili Dr.Masumbuko Lamwai na Wakili
Haraka.
Katika shauri hilo,dai la msingi la mlalamikaji
bwana Kiruswa lilikua ni
1.Kutumika kwa lugha ya matusi na kashfa wakati
wa kampeni kutoka kwa mh Onesmo Nangole
2.Kuwepo kwa wapiga kura kutoka nchi jirani ya
Kenya walioletwa na Mh Nangole
3.kutumika kwa magari ya Chadema kwenye
kusindikiza na kubebea masanduku ya kupigia
kura
4.Mkurugenzi wa Uchaguzi kutangaza matokeo
baada ya mgombea wa CCM kutolewa nje.
5.kutokea kwa vurugu ndani ya chumba cha
kuhesabu matokeo
Kutokana na madai hayo na kwa kuzingatia
kanuni,sheria na ushahidi uliotolewa pamoja na
vielelezo na mashahidi wa pande zote mbili,Jaji
kutoka mahakama kuu Bukoba Mh.Jaji Mwagesi
alisema;
“Kutokana na kuzingatia viini vyote vya shauri hili
kama vilivyosikilizwa na kwa mujibu wa
sheria,Natamka kwamba;
Mahakama hii imetengua shauri hili na kwa
kujirisha kwamba mchakato mzima haukuwa wa
haki."

Chapisha Maoni

 
Top