zichukuliwe dhidi ya kampuni nne za makandarasi
ambazo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul
Makonda alisimamisha zisipewe zabuni kutokana
na kazi nyingi walizopewa kuwa chini ya kiwango.
Kampuni hizo ni Inshinomya ambayo mkataba
wake umesimamishwa kutokana na uwezo wake
wa kujenga kuonekana kuwa mdogo, wakati
kampuni za Del Mononte, Skol Building
Contractors na Germinex Construction zikisitishiwa
kupewa zabuni mpya hadi watakapojiridhisha kuwa
wana uwezo.
Magufuli aliyasema hayo jana wakati wa uzinduzi
wa mpango wa usalama wa raia na kutaka Bodi ya
Usajili wa Makandarasi (CRB) na Bodi ya Usajili wa
Wahandisi (ERB) pamoja na Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuanza
kulishughulikia suala hilo kwa mujibu wa Sheria ya
16 na 17 ya mwaka 1997 ikiwa ni pamoja na
Injinia aliyekuwa akisimamia miradi yote ya
wazabuni hao naye pia kuchukuliwa hatua za
kisheria.
“Lazima twende mbele kwa yale tuliyoahidi
ninakupongeza RC kwa hatua anazochukua kwani
analalamika pamoja na vyombo vya dola kuwepo
na hawataki kuchukua hatua,” alisema Magufuli.
Akizungumza jana, Makonda alitoa mfano wa
barabara iliyojengwa kwa kiwango cha chini kuwa
ni ile inayotoka Ubalozi wa Ufaransa-Biafra mpaka
Mwananyamala.
Alisema makandarasi hao walilipwa zaidi ya Sh
bilioni nne na nyingine milioni 400 kinyume cha
utaratibu, hivyo aliagiza makandarasi hao kujenga
upya barabara hizo kwa fedha zao na zile
walizolipwa bila utaratibu wazirejeshe.
HabariLeo
Chapisha Maoni