0
Askari wa Jeshi la Ulinzi wa Wananchi Tanzania
(JWTZ) wa kambi ya Lugalo, Hamis Omary (31),
amefikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Kinondoni
akituhumiwa kumbaka mtoto (jina limehifadhiwa)
mwenye umri wa miaka minne.
Mbele ya Hakimu Caroline Kiliwa, wakili wa
Serikali, Amani Mghamba, alidai kuwa mtuhumiwa
alitenda kosa hilo Mei, 31 mwaka huu eneo la
Kawe, Wilaya ya Kinondoni.
Akisoma hati ya mashtaka, wakili Mghamba alidai
kuwa mtuhumiwa alifanya kitendo hicho
kilichomsababishia maumivu makali mtoto huyo.
Mtuhumiwa alikana shtaka linalomkabili na Hakimu
Kiliwa alisema kwa mujibu wa sheria shitaka hilo
lina dhamana hivyo alimtaka mtuhumiwa awe na
wadhamini wawili wanaotoka serikalini au katika
taasisi yoyote inayotambulika kisheria.
“Kila mdhamini anatakiwa aje na barua kutoka kwa
mwajiri wake kisha wataweka ahadi ya maandishi
ya Sh milioni 2 kwa kila mmoja,” alisema Hakimu
Kiliwa.
Mtuhumiwa alishindwa kutimiza masharti ya
dhamana na alirejeshwa mahabusu hadi Julai 8
mwaka huu ambapo kesi hiyo itatajwa tena.

Chapisha Maoni

 
Top