Nchemba ameitaka Polisi kutotumia nguvu kubwa
katika mambo yasiyokuwa na manufaa kwa
wananchi ila nguvu hizo zitumike kupambana na
biashara ya dawa za kulevya kwa maslahi
mapana ya taifa.
Nchemba ameyasema hayo juzi wakati akifunga
mafunzo ya awali ya polisi na uhamiaji, katika
Shule ya Polisi Tanzania-Moshi, ambapo zaidi ya
wanafunzi 3,000 walihitimu mafunzo hayo.
Alisema polisi ikifanya jitihada za kutokomeza
biashara na matumizi ya dawa ya kulevya, kila
Mtanzania kwa kabila lake, kwa rangi yake na
imani yake atalipongeza jeshi hilo kwa kazi
ambayo watakuwa wameifanya.
Alisema wananchi hawataweza kulipongeza jeshi
hilo kama litatumia nguvu kubwa ya kupambana
na masuala yasiyo na tija kwa wananchi, ambapo
aliwataka wahitimu wa mafunzo hayo kutekeleza
kwa vitendo yale yote waliyofundishwa kwa
mujibu wa taratibu za jeshi hilo.
Nchemba pia ameliagiza Jeshi la Polisi
kuwachukulia hatua kali za kinidhamu kwa mujibu
wa taratibu za jeshi hilo, askari Polisi wanaokiuka
maadili ya utendaji kazi wao, ikiwa ni pamoja na
askari wanaobambikia watu kesi, kupokea rushwa
pamoja na kukamata raia kwa kutumia nguvu
zisizostahili.
Alilaani pia tabia ya wananchi kujichukuliwa
sheria mkononi kama vile kuua watu wasiokuwa
na hatia kwa visingizio za imani za kishirikina,
pamoja na sheria kutofuatwa kwa watuhumiwa.
Mkuu wa Shule ya Polisi Tanzania- Moshi,
Matanga Mbushi, alisema wanafunzi hao
wamepewa mafunzo mbalimbali
yatakayowawezesha kufanya kazi kwa ufanisi na
kuongeza kuwa kati ya wanafuzi wanaohitimu,
wanafunzi 99 wametimuliwa kutokana na makosa
ya nidhamu na mimba.
Chapisha Maoni