Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, amesema
ugonjwa usiofahamika ulioibuka mkoani Dodoma,
unatokana na sumukuvu inayopatikana kwenye
nafaka.
Akizungumza jijini, Dar es Salaam jana, Ummy
alitolea ufafanuzi kuhusu ugonjwa huo na
kuongeza ndani ya wiki moja, kumekuwa na
ongezeko la wagonjwa 11 na kufanya jumla ya
wagonjwa kufikia 32, ingawa idadi ya vifo
haijaongezeka.
Alisema majibu kuhusu ugonjwa huo yanatokana
na uchunguzi wa awali uliofanywa na Mamlaka ya
Chakula na Dawa nchini (TFDA) na kwamba
serikali imechukua nafaka kadhaa zinazopatikana
mkoani Dodoma ili kuzipeleka Atlanta, Marekani
kwa uchunguzi zaidi.
“Tulitoa taarifa ya kuwepo kwa ugonjwa huo Juni
19 mwaka huu ambao ulipatikana wilaya za
Chemba na Kondoa, kulikokuwa na wagonjwa 21
na vifo saba, hata hivyo mpaka kufikia juzi
wagonjwa waliokumbwa na ugonjwa huo
wameongezeka na kufikia 32 na idadi ya vifo
imebakia saba,” alisema Ummy.
Alisema katika jitihada za kutambua kiini cha
ugonjwa huo, Wizara imepeleka jopo la
wataalamu huko Dodoma ili waweze kushirikiana
na wenzao walioko huko kufanya uchunguzi wa
kina wa ugonjwa huo.
Alisema sampuli mbalimbali za damu, haja
ndogo, haja kubwa, vinyama vya ini na sampuli
za vyakula, zilipelekwa katika maabara za Mkemia
Mkuu wa Serikali, maabara ya Mamlaka ya
Chakula na Dawa (TFDA), Maabara ya Taifa ya
Magonjwa ya Binadamu na maabara ya Hospitali
ya Rufaa ya KCMC ya Moshi mkoani Kilimanjaro.
“Vile vile sampuli nyingine kesho zitapelekwa
Marekani katika maabara ya Kituo cha Udhibiti wa
Magonjwa cha Marekani (CDC) kilichopo Atlanta
kwa uchunguzi zaidi,” alisema Ummy.
Aidha alisema, “kuna uwezekano mkubwa
kwamba ugonjwa huu umesababishwa na ulaji wa
chakula kilichokuwa na sumukuvu na kuleta
madhara, ili kuwa na uhakika na jambo hilo
Wizara yangu inasubiri matokeo ya vipimo vya
damu na haja ndogo vilivyopelekwa katika
Maabara ya CDC matarajio yetu ni kupata majibu
hayo katika kipindi kisichozidi wiki moja.”
Alisema tangu ugonjwa huo ulipoibuka, wagonjwa
12 wametibiwa katika Hospitali ya Mkoa wa
Dodoma na 18 wametibiwa Hospitali ya Wilaya ya
Kondoa.
Chapisha Maoni