0
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
YAH: UTEUZI WA MKURUGENZI MKUU WA
MAMLAKA YA
BANDARI TANZANIA (TPA)
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe.
Prof. Makame M. Mbarawa, leo tarehe 25 Juni,
2016 amemteua Mhandisi Deusdedit Conatus
Vitalis Kakoko kuwa Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Bandari Tanzania.
Mhandisi Kakoko amechukua nafasi iliyoachwa
wazi na Bw. Ephraim Mgawe ambae uteuzi wake
ulitenguliwa.
Mhandisi Kakoko ni Meneja wa miradi kutoka
Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS).
Uteuzi huu unaanza mara moja.
Ramsey V. Kanyanga
KAIMU KATIBU WA WAZIRI
25/06/2016

Chapisha Maoni

 
Top