0
Meneja wa Manchester City Pep Guardiola
anaamini ameshinda mbio za kumsajili beki wa
Everton John Stones, 22, lakini Chelsea na
Manchester United bado pia wanamfuatilia (Sun),
Kiungo wa Spain na Chelsea Cesc Fabregas, 29,
anasema uamuzi wa Uingereza kujiondoa kutoka
Umoja wa Ulaya utaathiri Ligi Kuu ya England
(Sunday Telegraph), meneja wa Arsenal Arsene
Wenger anatarajia kukutana na wawakilishi wa
mshambuliaji wa Lyn, Alexandre Lacazette, 25,
lakini anakabiliwa na ushindani kutoka Atletico
Madrid na West Ham (Sunday Mirror), meneja wa
Manchester United Jose Mourinho
anaghadhibishwa na mkakati wa usajili wa Old
Trafford kwa kumsajili beki mmoja tu Eric Bailly,
22, mpaka sasa (Manchester Evening News),
Manchester United watalazimika kuvunja rekodi ya
dunia ya pauni milioni 85.3 ambayo Real Madrid
walitoa kumsajili Gareth Bale, ikiwa wanataka
kumsajili kiungo wa Juventus Paul Pogba, 23
(Sunday Telegraph), Jose Mourinho ana uhakika
kuwa pauni milioni 30 zitatosha kumsajili winga wa
Wolfsburg Julian Draxler, 22, ikiwa atashindwa
kumpata Henrikh Mhkitaryan, 27 kutoka Borussia
Dortmund (Star on Sunday), Tottenham
wanakabiliwa na ushindani kutoka Paris St-
Germain kumsajili mshambuliaji wa AZ Almaar
Vinvest Janssen, 22 (L’Equipe), Bayern Munich
wamevutiwa na uchezaji wa kiungo wa Tottenham
Eric Dier, 22, kwenye michuano ya Euro 2016
(Sunday People), meneja mpya wa Everton Ronald
Koeman anataka kumsajili kiungo wa Manchester
United Morgan Schneiderlin, 26 (Sunday Mirror),
Stoke watakamilisha usajili wa mshambuliaji wa
West Brom Saido Berahino, 22 wiki hii (Sunday
People), Swansea wanakaribia kumsajili beki wa
kari wa Ajax Mike van der Hoorn, 23, kwa mkataba
wa pauni milioni 2 (Mail on Sunday), meneja wa
Newcastle Rafael Benitez anajiandaa kutoa dau la
pauni milioni 10 kumsajili kiungo wa Bournemouth
Matt Ritchie, 26, kutokana na wasiwasi kuwa
huenda Andros Townsend, 24, anaweza kuondoka
(Sun). 

Chapisha Maoni

 
Top