0
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda
amemsimamisha kazi Mhandisi wa Mkoa,
Josephat Shehemba kwa kushindwa kutimiza
wajibu wake, ikiwemo usimamizi wa barabara na
kusababisha kujengwa chini ya kiwango.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini
Dar es Salaam, Makonda alisema amefikia uamuzi
wa kumsimamisha kazi baada ya kuona injinia
huyo ameshindwa kutekeleza majukumu yake ya
usimamizi.
Alisema jukumu la usimamizi wa barabara,
unapaswa kuwa chini ya Shehemba, lakini
ameshindwa kufanya hivyo jambo lililosababisha
usimamizi huo kufanya na wananchi na wakuu wa
wilaya ambao sio kazi yao kufanya hivyo.
“Ni lazima alitakiwa kufanya kazi yake ya
usimamizi na kuhakikisha barabara zinajengwa
kwa kiwango kinachotakiwa lakini matokeo yake
kazi yake ameiacha na kufanya na watu wengine
ambao hawakupaswa kufanya hivyo,” alisema
Makonda.
Aidha, Makonda alisema kukosekana kwa
usimamizi mazuri wa kiongozi huyo
kumesababisha barabara nyingi za mkoa huo
kuwa chini ya kiwango na nyingine kuharibika
muda mfupi baada tu ya kutengenezwa.
“Ameshindwa kusimamia lakini anakuwa mtu wa
kwanza kudai fedha za kuwalipa wakandarasi
ambao wamejenga barabara chini ya viwango
angepaswa kusimamia atakapokwama au
kumuona mkandarasi ameshindwa kufanya kazi
yake kwa viwango basi angenieleza ili tuone
tunafanya utaratibu gani,” alisisitiza.
Makonda pia alisema ni jukumu la kila kiongozi
kutimiza wajibu wake, ikiwa ni pamoja na kuwa
msimamizi mkuu katika idara yake.
“Hatutomvumilia kiongozi yeyote atakayekwenda
kinyume na taratibu za kazi inavyomtaka kama
ameshindwa bora ahame mkoa kwa sababu hapa
kwangu sitamvumilia,” alisema.

Chapisha Maoni

 
Top