0
"Leo kwa maelekezo ya viongozi wakuu wa yanga,
nimetangaza mchezo wetu na TP mazembe kesho
hautakuwa na kiingilio ni BURE."
"Tunaombwa kuhamasishana sisi na watu wetu
wote wawahi uwanjani kwa wingi wakiwa na jezi,
bendera na vuvuzela na shamra shamra ili tuuteke
uwanja kwa kiasi kikubwa.
Hautakuwa na majukwaa ya simba wala yanga
tunakaa pamoja na wenzetu.
Lengo ni kwanza kuwaonyesha umma na wote
waliotaka kutuhujumu kwa mechi yetu kuwa sisi ni
yanga wa kimataifa na tunawapenda watu wote
japo baadhi wanatuchukia tuwaumbue kwa
kuwaonyesha upendo na furaha ili mwisho wa siku
wakubali kuwa yanga ni ya kimataifa.
Pili Tunaombwa kuhamasisha watu wetu
wasiwapige watu watakaovaa nguo nyekundu na
kukaa majukwaani na sisi tuwaache ili duniani ione
ukweli na wale wabaya wetu waumbuke.
Tunakwenda kupambana ndani ya uwanja
kikamilifu.
Na nje ya uwanja haswa tutakao kuwa majukwaani
tunaomba tushangilie kwa nguvu zetu zetu
mwanzo mwisho.
Tumejifunza kwa wenzetu waarabu jinsi
wanavyoshangilia pasipo kuchoka na sisi hivyo
hivyo tushangalie bila vurugu tunaomba sana.
Na mwisho mpira ukiisha tuhamasishana kutoka
taratibu na kurejea majumbani kwetu bila kufanya
vurugu."

Chapisha Maoni

 
Top