0
Msanii Nay wa Mitego ambaye siku si nyingi
anatarajia kuachia kazi yake mpya 'Pale kati
patamu' amesema kuwa baada ya kazi yake hiyo
kutoka itakuwa ni wakati sahihi yeye kutambulisha
rasmi wasanii walio chini ya Label yake ya 'Free
Nation 966'.
Akizungumza kwenye kipindi cha Friday Night Live
cha EATV, Nay wa Mitego alisema kuwa yeye ni
msanii wa kwanza kabisa kuanza kusimamia
wasanii wenzake, na sasa ameona awatambulishe
wasanii walio chini ya Label yake, ili afanye
biashara ya muziki na si kitu kingine.
"Unajua mimi ni msanii wa kwanza kuanza
kusimamia wasanii wenzangu, mpaka sasa nina
wasanii watatu ambao wapo chini ya Free Nation,
lakini kwa kuanza tutaanza na mmoja ambaye
tushakamilisha naye kila kitu anaitwa Tiki, nadhani
Label yangu itakuwa na utofauti na Label nyingi
sababu moja mimi ni mfanyabiashara hivyo hata
msanii naye mleta lazima aingizie pesa huku
akiwakonga mashabiki zake kwa muziki mzuri"
alisema Nay wa Mitego.
Hivyo tutaanza na Tiki huku tukiangalia biashara
yake inakwendaje, mimi sitaki kukurupuka nataka
kufanya biashara, hivyo baada ya kazi yangu
kutoka haitachukua muda atakuja Tiki kwa
watanzania, ingawa chini ya Free Nation kuna
wasanii watatu mpaka sasa" alisisitiza Nay wa
Mitego.

Chapisha Maoni

 
Top