0
Juni 26 mwaka huu Rais John Pombe Magufuli
alitangaza kuteua Wakuu wa Wilaya zote nchini,
na Wakuu wa Mkoa watatu. Kati ya Wakuu wa
Wilaya 139 walioteuliwa, 39 wamebakishwa katika
nafasi zao huku 100 wakiwa ni wapya.
Katika hali ya kushangaza siku moja baada ya
orodha hiyo kutangazwa, Rais Magufuli
ametengua uteuzi wa mkuu wa wilaya ya Ikungi
iliyopo mkoani Singida. Rais Magufuli alitengua
uteuzi wa Bwana Fikiri Avias Said ndani ya masaa
24 tangu uteuzi wake.
Sababu kuu ya Rais kutengua Uteuzi huu
ameisema leo hii wakati wa hafla ya kuwaapisha
Wakuu wote walioteuliwa, ni kwamba jina
lilikosewa, na kusema kwamba Mkuu wa Wilaya
halali wa Ikungi ni Bwana Miraji Mtaturu ambaye
ni Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa
wa Mwanza,

Chapisha Maoni

 
Top