0
Mshambuliaji wa klabu ya TP Mazembe ya DR
Congo Thomas Ulimwengu amesema wapinzani wao wa jana klabu ya Yanga bado ina nafasi ya kuingia nusu fainali ya
kombe la shirikisho barani Afrika kwa kuwa kuna mechi ambazo endapo watashinda watatimiza
lengo lao.
Ulimwengu raia wa Tanzania amesema kwa namna Yanga wanavyocheza wanaonekana wamejiandaa
kikamilifu japo kuwa kukosekana kwa uzoefu wa mashindano wa kimataifa kwa wachezaji wake
ndiko kunakopelekea kushindwa kupata matokeo.
Nyota huyo amekiri kukutana na wakati mgumu sana katika mchezo wa jana lakini wakaonesha nini
thamani ya wachezaji wa kulipwa jambo lililowapa
ushindi wa bao moja kwa sifuri wakiwa ugenini.
Mazembe imekamata usukani wa kundi A ikiwa
imejikusanyia alama sita kwenye michezo miwili
ya awali huku Yanga ikiendelea kushikilia nafasi ya
mwisho katika kundi lake.

Chapisha Maoni

 
Top