0
Timu ya taifa ya vijana chini ya miaka
17, Serengeti Boys imeanza vema katika
kuwania nafasi ya kushiriki michuano ya
Afrika ya vijana chini ya miaka 17 baada ya
kuitwanga Shelisheli kwa mabao 3-0.
Katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye
Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam,
Segengeti Boys ingeweza kupata mabao
mengi zaidi kama washambuliaji wake
wangekuwa makini.
Hata hivyo, walipoteza nafasi nyingi sana
na baadaye walionekana kuridhika na
ushindi huo.

Chapisha Maoni

 
Top