0
Serikali imesema licha ya kuingiza tani nyingi za sukari nchi lakini bado kuna tatizo la sukari katika baadhi ya maeneo ya katika makao makuu za
mikoa na wilaya kwa kuuzwa bei ya juu kuliko bei elekezi kwa hisia za kuwa bidhaa hiyo imeadimika
nchini.
Akizungumza wakati wa kuahirisha Bunge la 11 hii leo, Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim
Majaliwa, amesema kuwa hadi kufikia Juni 30 kiasi
cha tani elfu 63 za sukari zimeingizwa kati ya tani elfu 80 zilizokuwa zinahitajika kufidia pengo
lililopo.
Mhe. Majaliwa amesema njia pekee ya kuondokana na uhabari wa sukari uliokuwepo miaka yote ni
kuongeza uzalishaji wa sukari ya ndani kwa
kukamilisha mpango makakati wa maendeleo ya
sukari kwa miaka mitano ijayo.
Mhe. Majaliwa amesema kuwa serikali itaendelea kusimamia soko la sukari kuendelea kushuka ili
mlaji wa chini amudu kununua huku ikifanya tathmini ya mahitaji halisi ya sukari nchini
kutokana kuingiza kiasi kingi cha sukari lakini bado kumeonekana na upungufu mkubwa.
Waziri Majaliwa amesema moja kati ya Malengo yaliyopo katika mpango huo ni pamoja na
kuanzisha kwa viwanda vipya ambapo
vitaanzishwa viwanda vya kati vitatu pamoja na
kuanzisha viwanda vikubeas katika maeneo ya
Bagamoyo, Rufiji, Kigoma na Kidunda.
Aidha wataongeza tija ya uzalishaji wa miwa
inayolimwa na wakulima wadogo, kwa kuboresha
upatikanaji wa pembejeo, miundombinu ya umwagiliaji, na kuboresha mfumo wa uendeshajw wa vyama vya wakulima wa miwa.

Chapisha Maoni

 
Top