Mjini Dodoma amewataka wabunge wa upinzani
ambao wamesusia vikao vya Bunge tangu Mei 30
kuingia Bungeni na kuacha kususia vikao vya
Bunge kwani hakuna tija kwa Taifa.
Mhe. Majaliwa ameyasema hayo alipokuwa akitoa
hutuba ya kuhitimisha mkutano wa tatu wa Bunge
la kumi na moja.
“Kitendo cha baadhi ya waheshimiwa wabunge
kususia vikao vya Bunge hakitoi picha nzuri kwa
wananchi waliotuchagua kuwasilisha matatizo yao
katika Bunge hili, hivyo natoa rai kwa
waheshimiwa wabunge hao kutafakari upya
uamuzi wao na niwasihi kwa busara zao waingie
ili kwa pamoja na kwa ushirikiano tuweze kutoa
ushauri kwa Serikali,” alisema Mhe. Majaliwa.
Aidha Mhe. Majaliwa alitoa ufafanuzi juu ya Katiba
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka
1977 ambayo imetoa haki na kinga kwa
waheshimiwa wabunge ili kujadili na kuhoji
utendaji wa Serikali kwa uhuru bila mashaka
yoyote ya kuweza kushitakiwa wanapotimiza
wajibu wao wakiwa Bungeni.
Aliendelea kwa kusema kuwa kinga ya aina hiyo
haijatolewa kwa mwananchi yeyote yule Nchini ila
kwa Wabunge, hivyo basi hakuna mbunge
aliyefungwa mdomo labda aamue kujifunga
mdomo yeye mwenyewe.
Mhe. Majaliwa amesema kuwa Bunge
linaongozwa na Katiba, Sheria na Kanuni za
Kudumu za Bunge, hivyo ni vyema zikafuatwa
kuondoa manung’uniko yasiyo ya lazima na
endapo kuna utata katika jambo lolote ndani ya
Bunge zipo taratibu zilizowekwa na kanuni za
kufuata ili kupata ufumbuzi na si kwa kususa
kuingia Bungeni kwani hakuna tija kwa Taifa.
Wabunge wa upinzani wamesusia vikao vya
Bunge tangu Mei 30, 2016 mpaka leo Juni 30
ambapo Bunge limehitimishwa.
Aidha wabunge hao wamekuwa wakiingia Bungeni
kila asubuhi na jioni kisha kutoka mara tu Naibu
Spika Mhe. Dkt. Tulia Ackson anapomaliza
kusoma Dua maalum la kuliombea Bunge na
Taifa.
Chapisha Maoni