0
KLABU ya Manchester United
ya England imeanza
majadiliano na Juventus ya
Italia juu ya kiungo kumsajili
tena kiungo wake wa zamani,
Mfaransa Paul Pogba.
Kwa mujibu wa gazeti la
L'Equipe la Ufaransa, Pogba,
mwenye umri wa miaka 23
sasa, aliyeondoka Man United
kuhamia Juventus kama
mchezaji huru mwaka 2012
baada ya kukataa kuongeza
Mkataba chini ya kocha Sir
Alex Ferguson kutokana na
kutopewa nafasi ya kucheza,
sasa anaweza kurejea Old
Trafford.
Paul Pogba anaweza kurejea
Manchester United akiwa na
umri wa miaka 23 PICHA
ZAIDI GONGA HAPA
Chini ya Ferguson, Pogba
alicheza mechi saba tu za
kikosi cha kwanza Man
United, lakini sasa chini ya
kocha Mreno, Jose Mourinho
Mashetano hao Wekundu
wanataka kumrejesha Old
Trafford.
Na inasemekana Juve,
maarufu kama Kibibi Kizee
cha Turin haiwezi kumuuza
nyota wake huyo kwa dau la
chini ya Pauni Milioni 82.8..
L'Equipe limesema kwamba ,
kocha mpya wa Man United,
Jose Mourinho anataka
kutambulisha mfumo wa
4-3-3 msimu ujao na
anamtaka Pogba akachezea
pamoja na Nahodha Wayne
Rooney katika safu ya kiungo
katikati, pamoja na
mshambuliaji Zlatan
Ibrahimovic, Anthony Martial
na Henrikh Mkhitaryan
pembeni.

Chapisha Maoni

 
Top