0
Wachezaji wa Ureno
wakishangilia baada ya
mwenzao, Ricardo Quaresma
kufunga penalti ya mwisho
na kuiwezesha timu hiyo
kushinda kwa penalti 5-3
mchezo wa Robo Fainali ya
Euro 2016 dhidi ya Poland
usiku huu Uwanja wa Stade
Velodrome mjini Marseille,
Ufaransa. Robert
Lewandowski alitangulia
kuifungia Poland sekunde ya
100, kabla ya Renato
Sanches kuisawazishia Ureno
dakika ya 33. Wengine
waliofunga penalti za Ureno
ni Cristiano Ronaldo, Renato
Sanches, Joao Moutinho na
Luis Nani, wakati za Poland
zilifungwa na Robert
Lewandowski, Arek Milik
na Kamil Glik, huku ya Jakub
Blaszczykowski ikichezwa na
kipa Rui Patricio. Ureno sasa
itacheza na mshindi kati ya
Ubelgiji na Wales katika Nusu
Fainali Julai 6

Chapisha Maoni

 
Top