ameanzisha label yake mpya ‘Shilole
Entertainment’ ambapo pia amemsaini msanii
chipukizi aitwae ‘Amaselly’.
Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na video
yake ya wimbo ‘SayMyName’, amekiambia kipindi
cha Clouds E kinachoruka katika runinga ya Clouds
TV, kuwa ameamua kuanzisha label hiyo ili
kuwasaidia wasanii wenye vipaji lakini hawapati
nafasi.
“Yeah nimemsani Amaselly aka Gaucho, kwa
sababu ni msanii mwenye heshima, amenitafuta
kwa muda mrefu, Shilole nisaidie nisaidie, kwa
hiyo nikajifikiria, nikaamua kumsaidia,” alisema
Shilole
Pia Shilole amesema amemsaini msanii huyo
kupitia label yake mpya iitwayo Shilole
Entertainment.
Kwa upande wa Amasely alimshukuru Shilole kwa
uwamuzi wa kumsaidia huku akihaidi mambo
mazuri.
Chapisha Maoni