usalama barabarani (trafiki) ambaye hivi
karibuni alitukanwa na mke wa waziri wa
serikali ya awamu ya tano (jina kapuni), baada
ya kulikamata gari lake kwa kuvunja sheria za
barabarani, hatimaye amepandishwa cheo
ikiwa ni maagizo ya Rais Dk. John Magufuli.
Habari kutoka chanzo cha uhakika, zinasema
kuwa askari huyo ambaye alilikamata gari la
mke wa waziri huyo baada ya kuvuka sehemu
ya waendao kwa miguu eneo la Namanga jijini
Dar es Salaam, amepandishwa hatua moja
mbele, kutoka koplo hadi sajenti.
Kitendo hicho cha kulikamata gari hilo, bila
kujali utambulisho na matusi ya mwanamke
aliyedai kuwa mke wa waziri, kilimfanya Rais
Magufuli kumsifu na kumuona kuwa jasiri
kazini kwake, hivyo kuliagiza jeshi la Polisi
kumpa promosheni mara moja.
Juzi Jumapili, Uwazi lilimkuta trafiki huyo
akiongoza magari maeneo ya Makumbusho
katika lango la kuingilia daladala akiwa na
cheo kipya cha usajenti.
Alipoulizwa kuhusu kuula huko, Mbango alikiri
kutokea kwa jambo hilo na kumshukuru
Mungu pamoja na uongozi wa Jeshi la Polisi
kwa kumkumbuka, huku pia akilishukuru
gazeti hili kwa kukumbushia katika toleo lake
Na 993 lililoripoti juu ya kutotekelezwa kwa
amri ya Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi
na Usalama wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Chapisha Maoni