France, itachezwa Robo Fainali ya Pili ya
EURO 2016, Mashindano ya Mataifa ya Ulaya,
kati ya Wales na Belgium.
Mshindi wa Mechi hii ya Leo atatinga Nusu
Fainali na kucheza na Portugal ambao Jana
Usiku waliibwaga Poland kwa Mikwaju ya
Penati 5-3 huko Stade Velodrome Mjini
Marseille Nchini France kwenye Mechi
iliyochezwa Dakika 120 kufuatia Sare ya 1-1.
Kuelekea Mechi hii kila wa Kocha wa Timu
hizi, Chris Coleman wa Wales na Marc
Wilmots wa Belgium, wameonyesha ari kubwa
ya ushindi ingawa kila Kambi inakumbwa na
hali tofauti.
Belgium ndio wameathirika zaidi kwani
itawakosa Majeruhi Jan Vertonghen, ambae
ameumia Enka na hatacheza kwa Wiki 8, na
Thomas Vermaelen ambae yuko Kifungoni.
Nafasi zao zinaweza kuchukuliwa na Wawili
kati ya Laurent Ciman, Jason Denayer na
Jordan Lukaku.
Kwa upande wa Wales, hawana Majeruhi na
wapo tayari kufanya kile walichokifanya
kwenye Mchujo kuelekea Fainali hizi za EURO
2016 walipoweza kuzoa Pointi 4 dhidi ya
Belgium bila hata kufungwa Goli moja
walipopambana na Belgium wakiwa Kundi
moja.
Kwenye Mchujo huo, wote walikuwa Kundi B
na Belgium kufuzu kama Washindi wa Kundi
na Wales kushika Nafasi ya Pili na kwa Mechi
kati yao Belgium ilitoka 0-0 huko
King Baudouin Stadium, Brussels hapo
Tarehe 18 Novemba 2014 na Wales kushinda
1-0 Mechi ya Pili ya Marudiano iliyochezwa
Tarehe 12 Juni 2015 huko Cardiff City
Stadium, Cardiff na Gareth Bale kufunga Bao
hilo la ushindi katika Dakika ya 25.
Kwenye hizi Fainali za EURO 2016, Belgium
walifuzu Nafasi ya Pili toka Kundi E ambalo
walifungwa 2-0 na Italy na kuzichapa 3-0
Republic of Ireland na 1-0 Sweden huku
Raundi ya Mtoano ya Timu 16 wakiitwanga
Hungary 4-0.
Wales wao walitoka Kundi B ambalo waliibuka
Washindi kwa kuifunga Slovakia 2-1,
kufungwa 2-1 na England 2-1 na mwisho
kuitoa Russia 3-0 huku Raundi ya Mtoano ya
Timu 16 wakiitoa Northern Ireland 1-0.
Katika Mechi hii, kila Timu itampa mzigo
mzito Staa wao mkubwa kwa Belgium
kumtegemea mno Eden Hazard wa Chelsea
kuzifungua Difensi na kufunga na Wales
kumtumaini Staa wa Real Madrid Gareth Bale
kuwapa ushindi.
Uso kwa Uso
-Belgium wameshinda Mechi 5 kati ya 12
zilizopita wakati Wales wameshinda 4 na Sare
3.
VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
Wales: Hennessey; Gunter, Chester, Williams,
Davies, Taylor; Allen, Ledley; Ramsey, Bale;
Robson-Kanu.
Kuikosa Nusu Fainali akipewa Kadi ya Njano:
Davies, Ramsey, Taylor, Vokes
Belgium: Courtois; Meunier, Alderweireld,
Ciman/Denayer, J Lukaku; Witsel,
Nainggolan; Mertens/Carrasco, De Bruyne,
Hazard; R Lukaku.
Nje: Vermaelen (Kifungoni), Vertonghen
(Majeruhi-Enka)
Kuikosa Nusu Fainali akipewa Kadi ya Njano:
Meunier, Witsel, Fellaini, Batshuayi
REFA: Damir Skomina (Slovenia)
EURO 2016
Ratiba/Matokeo:
ROBO FAINALI
**Mechi zote kuanza Saa 4 Usiku Saa za
Bongo
Alhamisi Juni 30
(Stade Velodrome, Marseille)
Poland 1 Portugal 1 [Dakika 120: 1-1, Penati:
Poland 3 Portugal 5]
Ijumaa Julai 1
(Stade Pierre Mauroy, Lille)
Wales v Belgium
Jumamosi Julai 2
(Stade de Bordeaux)
Germany v Italy
Jumapili Julai 3
(Stade de France, Paris)
France v Iceland
NUSU FAINALI
**Mechi zote kuanza Saa 4 Usiku Saa za
Bongo
Jumatano Julai 6
(Stade de Lyon)
Portugal v Wales au Belgium
Alhamisi Julai 7
(Stade Velodrome, Marseille)
Germany/Italy v France/Iceland
FAINALI
Jumapili Julai 10
**Saa 4 Usiku, Saa za Bongo
(Stade de France, Paris)

Chapisha Maoni