0
Kocha Joseph Omog tayari ametua nchini na amemalizana na uongozi wa klabu ya Simba. Omog raia wa Camerooon amewasili saa 9 alfajiri
akitokea kwao Cameroon.
Omog aliyeipa ubingwa Azam FC mwaka 2014, anatarajia kuanza kuinoa Simba rasmi ndani ya
siku tatu kufuatia kuingia mkataba na klabu hiyo leo.
Kocha Jackson Mayanja raia wa Uganda ambaye
alikuwa na kikosi msimu uliopita, ataendelea kuwa
kocha msaidizi wa kikosi hicho.

Chapisha Maoni

 
Top