0
Jana akihitimisha bunge, naibu spika ametolea ufafanuzi utekelezaji wa mfumo wa kielektroniki wa utambuzi wa alama za vidole
(AFIS), hoja iliyojengwa kutokana na mkaguzi
wa hesabu za serikali(CAG) kwa kutokamilika
kwa mradi huo.
Agizo la bunge lilimtaka afisa masuhuli wa jeshi la polisi kuhakikisha mfumo wa AFIS unafanya kazi ndani ya kipindi cha miezi sita.
Ripoti ilieleza mfumo wa AFIS ulikuwa
unafanya kazi katika vituo 14 pekee kati ya
vituo 108 hivyo agizo la kamati halikuwa
limetekelezwa kikamilifu.
Spika ametoa agizo kwa serikali kuhakikisha
mfumo huo unafanya kazi ndani ya miezi
mitatu ili kuboresha uwezo wa jeshi la polisi
kuwa na utambuzi wa haraka wa wahusika wa
matukio ya kihalifu katika vituo vyote nchini.
Pili masuala yote yaliyobainika kuwa na dosari
za kiutendaji yapatiwe ufumbuzi haraka.
Spika anatarajia sasa suala hilo litafikia
mwisho na mdhibiti na mkaguzi mkuu wa
hesabu za serikali atafunga hoja yake baada
ya kujiridhisha na utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa.

Chapisha Maoni

 
Top