Fonte amedai kuwa Manchester United watajuta kumkosa Renato Sanches aliyeondoka Benfica kwenda Bayern Munich kabla ya Euro 2016Beki wa Ureno Jose Fonte amedai kuwa
Manchester United watajuta kumkosa Renato Sanches aliyeondoka Benfica kwenda Bayern
Munich kabla ya kaunza kwa Euro 2016.
Manchester United waliaminika kuwa mstari wa
mbele kuipata saini ya nyota huyo wa miaka 18, lakini ghafla mambo yakabadilika baada ya
Louis van Gaal kukosa uhakika wa mustakabali
wak.
Sanches amefunga goli la kusawazisha Ureno ikitoka sare ya 1-1 na Poland kabla ya kufuzu
nusu fainali Euro 2016 Alhamisi usiku,
mchezaji huyo wa Ureno alitupia penalty yake pia katika hatua hiyo ya matuta.
Nahodha wa Southampton Fonte amesema
Bayern Munich wana bahati ya mtende
kumpata Mreno huyo lakini Man United
watajuta. “Kuwa mchezaji wa Ligi ya Uingereza, kwa upande wangu naona walikosa mchezaji mahiri
mwenye kipaji. Ni kijana mzuri, anawasikiliza
wakongwe, anapenda kujiufunza, ambalo ni
jambo jema. Inapendeza kucheza naye na
atakuwa mtu muhimu kwa taifa lake kwa
hakika.” Alisema Fonte.
“Hana hofu. Hajali. Anautafuta mpira kila
sekunde. Ana nguvu na imara, Bayern Munich
wana bahati kuwa naye.”
Inaaminika Sanchez anaweza kuigharimu
Bayern ziada ya paundi milioni 50.
Goal.com
Chapisha Maoni