0
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
Katika wiki chache zilizopita, kumekuwepo migongano mingi kuhusiana na masuala ya klabu
ya Yanga (Young Africans Sports Club) ambapo haikuwa vyema kuyajibu au kuyajadili wakati klabu
hiyo ilikuwa ikikabiliwa na mashindano ya kimataifa.
Lakini kwa hivi sasa ambapo mambo yametulia, nimeona ni wakati mwafaka wa kuyaelezea kama
ifuatavyo:

1. TAARIFA YA MCHEZO KATI YA YANGA NA TP MAZEMBE
1.1. Ningependa kumshukuru Rais wa Shirikisho la
Miguu wa Miguu Tanzania (TFF) ambaye
amenipongeza nikiwa kama Rais wa Yanga
kutokana na mafanikio yaliyofikiwa na klabu hiyo katika mashindano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.
Hata hivyo, ningependa kuanza kwa kuelezea
kwamba mimi Si Rais wa Yanga bali Mwenyekiti,
na nikiwa Mwenyekiti wa Yanga, kwa niaba ya
klabu hiyo, ninazipokea pongezi hizo.
1.2. Hata hivyo, pongezi hizo zingepokelewa kwa
moyo mkunjufu zaidi na Yanga iwapo TFF ingeisaidia Yanga kama inavyotakiwa kufanya.
Mambo ambayo TFF ingeyafanya na kuimarisha
utendaji wa klabu hiyo ni pamoja na:
1.2.1. Kutoingilia ratiba ya ligi kuu mwaka jana
ambapo iliiruhusu Azam FC kufanya ziara ambayo
ilikuwa nje ya ratiba na hivyo kufanya mabadiliko
katika ratiba ya ligi, jambo lililotufanya kushindwa kujipanga vyema.
1.2.2. Ingetoa mjumbe wa masuala ya kisheria
kutoka TFF kwenda Yanga kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa klabu hiyo uliofanyika huko Angola
ambapo ujumbe wetu pamoja na wa vyombo vya habari, ulifanyiwa fujo na kupigwa na polisi wa
Angola.
Matokeo yake, badala ya kutuunga mkono katika kupeleka rasmi malalamiko yetu kwenda Shirikio
la Soka la Afrika (CAF), TFF lilikaa kimya.
1.2.3. Ilibidi itupe vifaa vya CAF vilivyotumwa kwa
ajili ya kutumika katika hatua za makundi kwa
wakati unaotakiwa, jambo ambalo halikufanyika na
kutufanya tuingie gharama ambazo hazikuhitajika
na kutusababishia adhabu kutoka CAF.
1.2.4. Ilibidi ichukue hatua kutokana na
kuonyeshwa kwa klabu yetu kadi nyingi mno za
njano (8) na kadi moja nyekundu katika mchezo wa kundi letu nchini Algeria dhidi ya klabu ya MOB.
1.2.5. Ingehakikisha inatuonyesha wazi tarehe na
muda wa mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya
TP Mazembe ambapo badala yake waratibu
waliamua kuupanga mchezo huo dhidi ya TP
Mazembe dhidi ya maslahi ya Yanga.
Hali hiyo ilizidi kuvurugwa kwa kufikiwa mkatabw wa siri na Azam TV wa kuurusha nchini Tanzania
mchezo huo wa Yanga wakati klabu ilikuwa imepiga hatua katika majadiliano ya shirika la
utangazaji ya TBC (ambao mwaka jana walikuwa wamepokea magari matatu kutoka China ili kuimarisha matangazo ya moja kwa moja ambayo
yaligharimu kiasi cha Shilingi bilioni 5 kwa kila
gari) kwa ajili ya kiwango kinachotakiwa katika
kurusha matangazo kimataifa.
1.2.6. Pia ilibidi kuipa Yanga fedha za CAF kwa
kufuzu kuingia katika hatua hiyo ya mashindano
ambayo ilifahamika kuwa ni Dola 15,000 za
Marekani; fedha za Kombe la FA katika mchezo wake na Azam FC; Zawadi ya VODACOM ya Ligi
Kuu, zote hizo zikisemekana kuwa ni kiasi cha Sh.
Milioni 500, ambazo iwapo zingelipwa na TFF
katika muda mwafaka, Yanga ingezitumia fedha
hizo kukabiliana na majukumu mbalimbali ya
fedha ikiwa ni pamoja na bonasi za wachezaji hadi
usajili wa wachezaji katika dirisha maalum la CAF,
na kadhalika.
1.3 Mahali ambapo klabu inasimama leo hii ni
kutokana na juhudi zake yenyewe na si kutokana
na ushirikiano au msaada wowote ambao Yanga
imeupata kutoka TFF ambapo Yanga kamwe
haikuutegemea na ambapo imeona waziwazi
kwamba TFF imeshindwa kuisaidia.
1.4 Uamuzi wa Yanga kuwaruhusu mashabiki wa
soka kuingia bure katika mchezo huo ili kuweza
kumpata mchezaji “halisi japokuwa wa kufikirika”
wa 12 si jambo jipya katika soka, japokuwa jambo
hilo limekwenda kinyume na matakwa ya TFF
ambayo ilitegemea kufanya makato mbalimbali
ambayo yamefutwa na Mamlaka ya Mapato nchini
(TRA).
Pamoja na hayo yote, kama TFF wanataka
kusimamia michezo yetu, basi wachukue gharama
zote za maandalizi kabla ya kwenda kwenye
michuano kama nauli, posho za wachezaji na
kadhalika, hesabu tutawapelekea hivi karibuni.
Tunammsihi Rais wa TFF asigeuke kauli yake
maana sisi tumewaachia kutafuta fedha kwa ajili ya
maandalizi ya mechi zinazokuja kulingana na
uzito, tunaamini hatageuka.
Tunashangaa CAF na TFF walikuwa wapi wakati
rais mstaafu Jakaya Kikwete katika mchezo wake
wa kwanza katika Uwanja wa Taifa alipowaruhusu
mashabiki kuingia bure?
Inabidi wafahamu pia kwamba tulipocheza huko
Angola na Algeria, mashabiki waliruhusiwa kuingia
viwanjani bure tulipocheza huko.
Sisi kama klabu tunawathamini mashabiki wetu
katika kututia hamasa wakati tunacheza.
Mimi mwenyewe nilitoa fursa hiyo huko Mwanza
miaka ipatayo kumi iliyopita wakati klabu ilicheza
dhidi ya El-Merreikh, na hapakuwepo na adhabu
yoyote kutoka CAF kutokana na hatua hiyo.
Je, TFF wanatufanyia hivi kama kutuadhibu
kutokana na kukosa mapato ambayo
yangeliwezesha kufanikisha sikukuu ya Idd el Fitri?
1.5 Uamuzi wa kuwaruhusu mashabiki kuingia
bure Uwanja wa Taifa ni jambo lenye busara
nyepesi kufahamika kwa mtu yeyote.
Katika mchezo huo ambao ulipigwa uwanjani hapo,
mapato yasingezidi Sh. 100 Milioni, na baada ya
makato yote ambayo yangehitajika kufanyika,
klabu ingejikuta imebaki na kiasi cha Sh. 40
Milioni.
Hii ni kwa kuchukulia kwamba pasingefanyika wizi
wowote kwenye milango na pasingekuwepo na
tiketi bandia, hali ambayo hufanywa katika
michezo ambayo husimamiwa na TFF hasa ile ya
ligi.
1.6 Binafsi niliamua kwamba kwa vile Uwanja wa
Taifa ulikuwa umekodishwa kwa ajili ya
maonyesho ya starehe kwa Sh. 20 Milioni ambapo
kwa uelewa wangu kiasi hicho kilikuwa kimefutwa
na Waziri wa Michezo na Utamaduni kwa kuwa
Yanga ilikuwa inawakilisha taifa.
Klabu iliona ingebeba gharama zingine mbalimbali
zenye kuhusika na mchezo huo, yote hayo kwa
ajili ya kutaka mashabiki wengi wa Tanzania
waingie ili kuitia moyo Yanga katika siku hiyo ya
mchezo.
Niliongea na vyombo vya usalama, akiwemo Waziri
wa Mambo ya Ndani kuhusu nia hiyo ya Yanga,
ambapo jeshi la polisi lilifanya kazi nzuri sana.
Hali ya uwanjani ilikuwa tulivu kabisa isipokuwa
nje ambako baadhi ya mashabiki waliuziwa tiketi
feki ambazo tunahisi zilikuwa zimetayarishwa na
TFF.
Hata hivyo, polisi waliweza kudhibiti hali hiyo
ambapo hakuna aliyejeruhiwa au kukamatwa,
jambo ambalo linaonyesha wazi kwamba woga wa
CAF wa kuiadhibu Yanga kutokana na
kinachodaiwa vurugu, ni upuuzi mtupu.
1.7 Kuhusu suala la kutakiwa mashabiki 40,000
pekee waingie katika uwanja huo wenye kubeba
watu 60,000, jambo ambalo lilizua sababu kutoka
CAF kuiadhibu kwa kuipiga faini Yanga,
ninashangaa ni busara gani ilitumiwa na serikali
katika kujenga uwanja wa kuingiza watu 60,000 na
badala yake kutegemea uingize watu 40,000 tu!
Rais wa TFF hakupewa habari za kweli.
Ninachofahamu ni kwamba mratibu wa mechi
alisema kwamba maofisa wa TFF walitaka waingie
watu 40,000 tu ili kuipunguza nguvu Yanga lakini
alikataa, kwani hakuona sababu ya watu kuingia
na kuujaza uwanja kama ilivyo kawaida.
Isitoshe, Kamishna huyo ninaweza kumleta mbele
ya Watanzania wasikie jinsi TFF ilivyokuwa
inajaribu kumpotosha dhidi ya Yanga kwa vile
klabu hiyo ilikuwa imeamua kuionyesha mechi
hiyo bure na kuvinyima fursa vituo fulani vya
televisheni kuuonyesha mchezo huo, pamoja na
kuvuruga mipango ya TFF ya kupata fedha
kutokana na mauzo ya tiketi.
Katika hili, nina fahari kubwa kwa kutoa fursa kwa
zaidi ya mashabiki 60,000 kuiona mechi hiyo bure
ambayo hata kama hatukushinda lakini tulikuwa
pamoja kama Watanzania.
1.8 Nawajulisha wananchi kwamba uhasama kati
ya TFF na Yanga si mpya kwani hata katika
uchaguzi tuliofanya majuzi, kulikuwa na majaribio
ya kutaka kuvuruga matokeo yake, na njama hizi
zimefikishwa katika Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa (Takukuru).
Ni vyema TFF ikashughulikia matatizo yake
mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupanga matokeo
ya mechi mbalimbali, kuingilia masuala ya klabu
mbalimbali kama ilivyofanywa kwa Yanga kwa
kujaribu kutumia katiba ya zamani ya mwaka
2010, kuingia mikataba ya siri na wadhamini wa
ligi, haki za vituo vya televisheni kuonyesha mechi
na kusababisha kuziua klabu kifedha, na kujifanya
kuchukua hatua za maendeleo katika soka kwa
unafiki wa kutegemea kodi mbalimbali kutoka
Yanga na Simba.
Sisi katika klabu ya Yanga tuliokuwa katika Kamati
ya Utendaji hatuchukui hata posho za vikao kwani
tunataka kwanza kuifanya klabu ijitegemee kifedha
kabla ya maslahi yetu binafsi.
Kinyume chake, posho ndani ya TFF limekuwa
jambo la kawaida, hali ambayo imefanya hata
mahesabu yake yasichapishwe kwa ajili ya
kupitiwa waziwazi na kila mtu.
1.9 Nasisitiza kwamba katika uchaguzi uliofanyika
majuzi, kabla ya hapo nilikuwa Mwenyekiti nikiwa
nimechaguliwa kwa kura kwa kipindi cha miaka
miwili katika uchaguzi mdogo nikiwa nimeapa
kuleta uaminiano kati ya mashabiki na viongozi wa
klabu, ambapo kipindi hicho kiliongezwa baadaye
kwa mwaka mmoja na wanachama wa klabu, na
kuongezwa tena kwa mwaka mmoja kutokana na
kufanyika uchaguzi mkuu mwaka jana kutokana na
ushauri wa maandishi wa TFF.
Nimesema wazi kufuatia uchaguzi wa majuzi
kwamba nitapigania maendeleo ya klabu kwani
hapatakuwa na cha kufurahia na kuleta amani na
utulivu katika klabu iwapo Yanga itashindwa
kushiriki katika michuano ya soka barani Afrika,
jambo ambalo mashabiki wa Yanga wanalitaka siku
zote.
1.10 Pia ninanyoosha mkono wa urafiki kwa klabu
ya Simba kwa uchaguzi wao, japokuwa wao
hawakufanya hivyo niliposhinda. Nimeelekeza
kwamba utani (ushindani) kati ya Simba na Yanga
uwe katika viwanja vya soka, ndiyo maana katika
mechi yetu na TP Mazembe niliwakaribisha kama
Watanzania wenzetu, tuliwaheshimu wote pamoja
na wale waliovaa majezi na kuishangilia TP
Mazembe.
1.11 Mkono huo wa kutakiana mema sitaki
ubadilike na kuwa ngumi, bali uendeleze
ushirikiano, na TFF iache njama zake dhidi ya
Yanga bali iungane nasi katika kujenga soka la
Tanzania.
2. KUITWA KWA JERRY MURRO KATIKA KAMATI YA
MAADILI YA TFF AKIWA MKURUGENZI WA HABARI
WA KLABU
2.1. Hati za TFF za kuitwa kwa Jerry Murro
hazionyesha wazi sababu ya Mkurugenzi wa
Habari huyo wa Yanga kutakiwa kufanya hivyo
ambapo atakuwa akihudhuria si kwa cheo chake
katika klabu, lakini ifahamike wazi kwamba Yanga
haitakubali Mkurugenzi wake wa Habari afungiwe
kushiriki katika shughuli za soka.
Tukiwa kama klabu tuko tayari hata kuunga mkono
hatua zozote za kisheria dhidi ya TFF na iwapo
TFF itajaribu kuifungia Yanga, tutalichukua suala
hili hadi katika vyombo vya juu zaidi vya michezo.
2.2. Hata hivyo, iwapo kuitwa huko kunahusu
suala la faini ya Sh. 5 Milioni dhidi ya Jerry, fedha
hiyo ilikwishatolewa kwa TFF.
2.3. Wanaokula njama ndani ya TFF
kuwanyamazisha au kuwafungia ambao wanaeleza
mawazo yao kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania,
lazima wafahamu kwamba kuikosoa TFF
hakupingani na sheria, na wafahamu pia kwamba
Yanga chini ya uenyekiti wangu haitakubali
wanachama au wafanyakazi wa klabu kudhalilishwa
au kutishwa.

3. MKATABA WA TBL NA YANGA
3.1. Mkataba wa kampuni ya bia nchini (TBL) na
YANGA ulisainiwa miaka mitano iliyopita na
mtangulizi wangu. Huu ulikuwa mkataba haramu
kwani mamlaka ya kutia saini mikataba kwa
mujibu wa Katiba ya Yanga yapo kwa wadhamini
na hapana kitu kama azimio kutoka bodi ya
wadhamini kuingia katika makubaliano kama haya,
au mkataba kusainiwa na wadhamini.
3.2. Wakati wa kipindi changu kilichopita,
nilijitahidi kurekebisha tofauti zote zilizokuwepo,
lakini nilishindwa.
TBL ni mara moja tu imetoa mara moja tu Sh. 20
Millioni kwa ajili ya tamasha la Yanga Day
zilizoahidiwa kutolewa kila mwaka, haijailipa klabu
fedha ya marekebisho inayofikia Sh. 30 Milioni
wala haijatupa basi kwa kiwango sahihi tulichotaka
kama ililoahidi katika mkataba.
TBL imejulishwa kuhusu hili lakini
haijalishughulikia.
3.3. Yanga imeingia katika mkataba wa masoko na
kampuni ya International Marketing ili kupata
wafadhili wake, ili kupunguza pengo la TBL kwa
ajili ya mishahara ya Juni.
Hii ni kampuni ambayo nilikuwa mwenyekiti wake
na ikakubali ufadhili huo wa mwezi mmoja, jambo
ambalo liliifanya Yanga kuvaa jezi za nembo yake
katika mchezo dhidi ya TP Mazambe.
3.4. Iwapo wanachama wa Yanga wakihisi nilivunja
katiba kwa maslahi yangu binafsi au wakiwa na
sehemu nyingine bora zaidi ya kufanya hivyo,
walifikishe suala hilo kwenye kamati ya maadili ya
klabu kwa ajili ya uamuzi.

4. MUHTASARI
4.1. Nimechaguliwa katika mazingira ya amani
zaidi miongoni mwa vyama vya soka nchini na
ambapo hakuna hata senti moja ilitumika kwa ajili
ya kumhonga yeyote.
4.2. Nilisimama bila kupingwa kugombea nafasi ya
Mwenyekiti na nikawaambia wapiga kura wangu
waziwazi kwamba:
Wakati huu nikiwa Mwenyekiti sitakaa kimya kwa
wale watakaojikita katika kuhujumu masuala ya
fedha klabuni na wale wanaoamini kwamba TFF iko
juu ya sheria zinazohusu masuala ya biashara na
haihusiki na Katiba ya Tanzania.
Nawashukuru wapiga kura wangu ambao
walinipigia kura kwa asilimia 100 ya ushindi
wangu.
4.3. Masuala yanayotokea uwanjani au usajili wa
wachezaji ni ya soka na kwamba TFF ina mamlaka
ya kuipeleka mbele nchi yetu kwa kufuata
miongozo ya FIFA.
Lakini sitavumilia upuuzi wa TFF kutaka kuingilia
masuala ya Yanga. Tunajua FIFA imechafuka kwa
rushwa na kusababisha Sepp Blatter kuong’olewa
na kukabiliwa na mashitaka: hata hivyo, iwapo
tungetumia kauli za TFF, Blatter na Platini
wasingefanywa chochote.
Masuala ya fedha ya klabu yetu, yawe kuhusu
nembo ya klabu kwenye kituo cha televisheni bila
ya kibali cha Yanga si ya kuamuliwa na TFF.
Kilichopo ni kwamba kitu cha televisheni
kinatengeneza fedha kutoka kwa Yanga, TFF
inatengeneza fedha kutoka kituo cha televisheni.
Hivyo, iwapo kuna mtu anafikiri sijui sheria za
mashindano bora ya kibiashara na hakimiliki, basi
wajue hilo litawagharimu.
4.4. Iwapo TFF inataka Mwenyekiti wa Yanga
akubaliane na uwongo, basi katika miaka minne
ijayo niko tayari kupambana na uovu huo na
kusahihisha kila kitu. Hata hivyo, kwanza kabisa
niko tayari kushirikiana kirafiki na wakati huohuo
kupigania haki za klabu kwani daima nimekuwa
mtu mwenye kupigania haki na masuala ya
kikanuni ninayoyaamini ni ya kiadilifu.
4.5. Yanga ilikuwepo kabla yangu na itakuwapo
baada yangu. Ni wajibu wangu kuiacha Yanga
ikiwa klabu bora zaidi kuliko nilivyoikuta na
nikiona siwezi tena kutumikia maslahi ya
wanachama wake, sitasita kujiuzulu au kuitisha
uchaguzi ili kujipanga upya.
5. MWISHO:
5.1. Kwa mashabiki wa soka wa Yanga na
Tanzania nzima, tumefikia hatua ya makundi ya
Kombe la Shirikisho si kwa bahati.
Mwaka jana tulitolewa kwa tofauti ya mabao ya
kufunga. Na mwaka huu tumekutana na uhasama
katika mechi zetu ambapo tulipigwa mabomu ya
machozi, mbali na huko Misri ambako tulifanyiwa
njama mbalimbali. Vilevile TFF nayo imekuwa
haitupi msaada wowote bali kutuhujumu tena.
Nasema sitavumilia hujuma hizi dhidi ya Yanga.
5.2. Sisi ni klabu ambayo tumejaa ujasiri,
hatujalipiza kisasi kwa tulichofanyiwa wapinzani
wetu wakija hapa.
Ndiyo, tumeshindwa mechi mbili, lakini kwa
heshima.
Hatutashusha vichwa vyetu kwa aibu au kutaka
kufanikisha mambo yetu kwa njia za panya.
Tutawekeza katika timu yetu kila raslimali.
Natoa wito kwa Yanga kutokata tama katika juhudi
za kujenga uwanja wetu juu ya misingi aliyoiacha
Mzee Karume.
Tusisahau kwamba tulikuwa msingi wa nguvu
zilizomfanya Mwalimu Nyerere kuikomboa
Tanzania na nchi nyingi za Afrika.
Historia yetu imejaa kila aina ya fahari.
Tumepigania yote tuliyoyaamini na tumeshinda.
Matumaini yetu ya kutwaa kombe la ushindi wa
ubingwa katika Afrika yako karibu na kwamba kila
hatua tufanyayo inatupeleka karibu na lengo hilo.
Mustakabali wetu unatuonyesha kwamba kama si
mwaka huu, basi mnamo miaka mitatu ijayo
tutafika katika fainali za michuano hii tukishirikiana
vyema.
Ni kweli wasaliti wapo, lakini lazima tusonge
mbele, kila tunapokatishwa na tama na watu
wengine, basi tujue tunakaribia ushindi wetu.
5.3. Nataka kila mtu aamini kwamba hii ni timu
yake si yangu mimi.
Tunamtaka zaidi kila mtu hivi sasa kwani
tunakaribia katika lengo letu la kutwaa ubingwa wa
Afrika, japokuwa tunafahamu kwamba kuna mengi
ya kufanya lakini mengi zaidi tumeishamaliza,
kikubwa matunda yanaonekana na tunashiriki
michuano ya kimataifa tunashiriki na tunapiga
hatua moja mbele.
5.4. Si rahisi lakini tusilalamike. Hakuna kitu
Mungu anatuwekea mbele yetu bila ya sisi kuwn na nguvu ya kuvuka.




Kwa imani, DAIMA MBELE, NYUMA MWIKO.
Asante.
(YUSUF MEHBUB MANJI)
MWENYEKITI WA KLABU YA YANGA

Chapisha Maoni

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top