0
MKUU wa kitengo cha Habari na Mawasiliano cha klabu ya Yanga,Jerry Muro,amesema mwenye
uwezo wa kumwambia akae pembeni ni mwajiri wake ambaye ni Yanga na siyo mtu mwingine.
Muro ametoa kauli hiyo kupitia kipindi cha Michezo kinachorushwa na kituo cha Redio cha TBC Taifa alipotafutwa kuongelea kifungo cha mwaka mmoja alichopewa na TFF jioni ya leo.
Amesema TFF haina uwezo wa kumfungia kwani
yeye siyo mwanachama wala mwajiriwa wa shirikisho hilo.
Muro akiongea toka kijijini kwao Machame,mkoani Kilimanjaro,ameongeza kuwa hatambui kufungiwa huko na kusisitiza kuwa kama TFF wanataka
kumfungia mtu basi waifungie Yanga kwani ndiyo
inayomtuma kusema anachokisema.
Jioni ya leo Kamati ya maadili ya TFF imetangaza
kumfungia Murro Kutojihusisha na masuala ya soka kwa kipindi cha mwaka mmoja pamoja na
kumlima faini ya shilingi milioni tatu kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kupingana na maagizo ya shirikisho hilo. 

Chapisha Maoni

 
Top