baada ya Chelsea kukubali mziki wa kiungo wake matata kabisa, mkata umeme, N'Golo Kante na hivyo kumwaandalia mkataba mpya wa miaka mitano na mshahara wa Pauni 290,000 kila wiki.
Habari ndiyo hiyo. Chelsea inafanya hivyo ili kuwakata kilimilimi wale wanaomfukuzia kiungo wake huyo, hasa Paris Saint-Germain, ambayo inaonekana udenda kuitoka ikiitaka huduma yake.
Mkataba wa sasa uliobaki huyo Stamford Bridge ni miaka miwili, lakini kwa dili hilo jipya ambalo litamfanya aweke kibindoni Pauni 75 milioni litakwenda kukomea mwaka 2023.
Mshahara huo mpya utamfanya Kante kulipwa pesa nyingi zaidi, zaidi ya Pauni 70,000 anazolipwa Eden Hazard, ambaye pia anaweza kusainishwa dili jipya ili kumfanya asishawishike kwenda Real Madrid.
Mabingwa wa Ufaransa PSG wamemweka Kante kwenye chaguo lao la kwanza la wachezaji inaowataka, lakini kocha mpya wa Chelsea, Maurizio Sarri anataka kubaki na wachezaji wake wote bora akiwamo Hazard na Willian katika msimu wake wa kwanza.
Lakini shida inayowakabili Chelsea ipo kwa kipa Thibaut Courtois, ambaye ameripotiwa kuwaambia wababe hao wa London wakubali tu kumuuza kwenye dirisha hili la sivyo ataondoka bure mwakani.
Chapisha Maoni