Timu ya Simba imepata sare ya bao 1-1 dhidi ya wapinzani wao Mouloudia mechi ambayo imevunjika dakika ya 65 kutokana na mvua inayonyesha. Adam Salamba ameifungia timu yake bao katika dakika ya 61 na kufanya matokeo kuwa Simba 1-1 Mouloudia.
Simba iliyocheza mfumo wa 4-4-2 imekuwa na maelewako kuanzia kwenye ulinzi hadi ushambuliaji.
Kwenye ulinzi Wawa na Kotei walikuwa na maelewano mazuri kwenue viungo na washambuliaji kwa Kagere na Okwi.
Dakika ya 15 Simba walipata faulo lakini Emmanuel Okwi akapaisha.
Dakika ya 20 Aishi Manula ameokoa mpira wa hatari.
Kikosi cha Simba kilichoanza, Aishi Manula, shomari Kapombe, Asante Kwasi, James Kotei, Sergio Wawa, Jonas Mkude, Shiza kichuya, Chama, Meddie Kagere, Emmanuel Okwi na Hassan Dilunga.
Chapisha Maoni