Alexandre Lacazette akishangilia baada ya kuifugia Arsenal bao la kusawazisha dakika ya 90 ikitoa sare ya 1-1 dhidi Chelsea katika mchezo wa kirafiki wa Kombe la Mabingwa wa Kimataifa Uwanja wa Aviva mjini Dublin.
Alikuwa Antonio Rudiger kuanza kuifungia The Blues dakika ya tano tu ya mchezo huo. Arsenal ikaenda kushinda kwa penalti 6-5 baada ya Ruben Loftus-Cheek wa Chelsea kukosa penalti ya mwisho na Alex Iwobi kufunga kwa upande wa Arsenal, ambao wapo chini ya kocha mpya kwasasa Mspaniola, Unai Emery aliyechukua nafaisi ya Mfaransa, Arsene Wenger mwezi uliopita.
Waliofunga penalti za Arsenal ni Alexandre Lacazette, Reiss Nelson, Matteo Guendouzi, Ainsley Maitland-Niles, Mesut Ozil na Alex Iwobi wakati za Chelsea zimefungwa na Danny Drinkwater, Tammy Abraham, Victory Moses, Emerson na Lucas Piazon
Chapisha Maoni