0
Watu kadhaa wamepoteza maisha huku wengine wakijeruhiwa asubuhi hii kwenye ajali ya basi la Wibonela lililokuwa likitoka Kahama kwenda Dar
lililopinduka eneo la kona ya Phantom, Kahama.

Chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi uliopelekea dereva wa basi kushindwa kulimudu lilipofika kwenye kona ya Phantom na kupelekea kuingia
mtaroni na kupinduka.

Idadi kamili ya waliopoteza maisha na majeruhi kwenye ajali hiyo bado haijafahamika.
Baadhi ya miili tayari imetolewa katika eneo la ajali huku majeruhi nao wakikimbizwa kwenye Hospitali ya Wilaya Kahama kwa matibabu.



Katika hatua nyingine, mtu mmoja
amechomwa moto na wananchi wenye hasira kali baada ya kunaswa akiwaibia Majeruhi badala ya kutoa msaada.

Chapisha Maoni

 
Top