John Magufuli kutokana na ahadi yake ya kurejesha mali za Waislamu.
Lakini Sheikh Ponda hajakubaliana na kitendo cha Rais kutoa fedha taslimu kwa ajili ya kuchangia
safari za Hija, akisema mkuu huyo wa nchivangezungumza na wahusika ili kujua matatizo
ambayo fedha hizo zingesaidia.
Sheikh Ponda amesema ahadi hiyo ya Rais ni ya
kuungwa mkono kwa kuwa inaonyesha kujali masilahi ya wananchi, hususan Waislamu.
Juzi, akihutubia Baraza la Idd el Fitr jijini Dar es
Salaam, Rais Magufuli alisema atawasaidia Waislamu kurejesha mali zao na kumpongeza
Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu, Abubakar Zubeir
kuwa alikuwa mstari wa mbele katika kurejesha mali hizo kabla hata hajapewa cheo hicho.
“Nakumbuka wakati nikiwa Waziri wa Ardhi, kabla
hujawa Mufti, pamoja na viongozi wa Bakwata na wengine, ulifika ofisini kwangu ukieleza jinsi mali
za Waislamu zilivyokuwa zinadhulumiwa.
"Ninafamu pamekuwa na hiyo tabia ya baadhi ya viongozi wenye mali kuwatumia viongozi wa
Bakwata na dini nyingine katika kuwarubuni na
kuingia ubia. Mali hizo baadaye huwa zinapotea kabisa,” alisema.
“Tujitahidi kwa nguvu zote kusimamia mali hizi zisije kuwa chanzo cha kuvunjika kwa amani.
Tunapenda wawekezaji, lakini wanachokiahidi
hawatekelezi. Haiwezekani.
“Haiwezekani na wala haikubaliki kwa watu kwa ujanja wao na wakati mwingine kwa kutumia
wanasheria wao kukalia mali za Waislamu. Mali
za Waislamu lazima zirudi na za Wakristo zirudi
ili amani iwepo.”
Sheikh Ponda alisema kwa kauli hiyo, Rais Magufuli ametambua juhudi ambayo wamekuwa wakizifanya katika kupigania mali za Waislamu,
kama ilivyokuwa katika kupigania kiwanja cha Chang’ombe hadi kusababisha kesi dhidi yake na
wenzake.
“Utakumbuka, tulikuwa na kesi kuhusu kiwanja
cha Waislamu kule Chang’ombe, katika hatua za
awali tulishindwa, lakini baadaye tukakata rufaa na
kushinda. Ndiyo sababu ya kuunga mkono kauli
hii ya Rais,” alisema Sheikh Ponda.
Akizungumzia msaada wa Rais Magufuli kwa ajili
ya Hija, alisema hiyo ni ruzuku muhimu, lakini
Rais angekaa na Waislamu wamweleze mambo ambayo ni muhimu zaidi ili uwekezaji wake uwa na manufaa zaidi.
Alipoulizwa ni mambo gani ni muhimu zaidi, Sheikh Ponda alisema ni masuala ya elimu na
afya ambayo Serikali ikisaidia baadaye
yatapunguza mzigo mkubwa kwake.
Chz
Mpekuzi blog
Chapisha Maoni