Na Mwandishi wetu.
MKOA wa Mwanza kwa kipindi chaa
mwezi Juni mwaka huu umekuwa shwari
ikilinganishwa na ya mwezi mei mwaka
huu. katika matukio ya uhalifu.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa
Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi
amesema kuwa pamoja na kuwa usalama
kulikuwepo na baadhi ya matukio makubwa
ya jinai kama mauaji,unyang’anyi wa
kutumia silaha, unyang’anyi wa kutumia
nguvu, uvunjaji,kubaka na wizi wa mifugo.
Amesema licha ya kuwepo kwa hata hivyo
matukio ya uhalifu yaliweza
kushughulikiwa na jeshi la polisi
wakishirikiana na wadau wa ulinzi na
usalama vizuri, kwani baadhi ya
watuhumiwa wa uhalifu walikamatwa na
kufikishwa mahakamani, ambapo baadhi ya
kesi zimemalizika na nyingine zinaendelea
katika hatua tofauti mahakamani.
Taarifa hiyo ilisema kuwa watuhumiwa
walioguswa na ushahidi na kukimbia
baada ya kutenda matukio ya uhalifu
wanaendelea kutafutwa na jeshi la polisi
kwa kushirikiana na vyombo vingine vya
dola pamoja na wananchi wenye nia njema
ya kukabiliana na uhalifu katika mkoa
wetu wa mwanza.
Katika matukio katika kipindi cha mwezi
juni, 2016 jumla ya makosa 3753
yaliripotiwa, wakati kwa mwezi mei, 2016
makosa 3798 yaliripotiwa, hivyo
kunaupungufu wa makosa 45, sawa na
asilimia 1.2%.
Makosa yaliyotikisa makosa makubwa kwa
kipindi cha mwezi juni, 2016 yalikuwa ni
232 ikilinganishwa na ya mwezi mei, 2016
ambapo makosa makubwa 197
yaliyoripotiwa, hivyo kunaongezeko la
makosa 35 ambayo ni sawa na asilimia
15.8%, aidha katika kipindi cha mwezi
juni,2016 makosa madogo yaliyoripotiwa ni
3521 ikilinganishwa na mwezi mei, 2016.
Makosa ya Kawaida madogo 3601
yaliripotiwa, hivyo kunaupungufu wa
makosa 80, sawa na asilimia 2.2%. hata
hivyo upungufu huo unatokana na jitihada
za jeshi la polisi kubuni na kutumia mbinu
mpya za kupambana na uhalifu ambao
umekua kutokanana kukua kwa teknologia
pamoja na mbinu za kihalifu.
Makosa yanayotokana na jitihada za jeshi
la polisi wakishirikiana nawadau wa ulinzi
pamoja na wananchi kupitia misako na
doria, makosayapatayo 108 yaliripotiwa
katika kipindi cha mwezi juni, 2016
ikilinganishwa na mwezi mei, 2016 ambapo
makosa 77 yaliripotiwa, hivyokufanya kuwa
na ongezeko la makosa 31 sawa na
asilimia 29%.
makosa makubwa na madogo ya usalama
barabaranikwa upande wa makosa ya
usalama barabarani jumla ya makosa yote
yaliyoripotiwa mkoani mwanza katika
kipindi cha mwezi juni, 2016 yakiwemo
makosa ya ukiukwaji wa sheria za usalama
barabarani na usafirishaji ni 11,100
ikilinganishwa na mwezi mei, 2016
ambapoyaliripotiwa jumla ya makosa
10,490, hivyo kunaongezeko la makosa 1,390
sawa na asilimia 12.5% matukio ya ajali za
barabarani yaliyoripotiwa kwa kipindi cha
mwezi juni ni 12, ikilinganishwa na mwezi
mei, 2016 matukio yaliyoripotiwa yalikuwa
13 hivyo kunaupungufu wa tukio 01 sawa
na asilimia 08%. matukio ya ajali za vifo
yaliyoripotiwa kwa kipindi cha mwezi
juni,2016 ni 10.
Amesema ikilinganishwa na mwezi mei 2016
ambapo pia yalikuwa 10.watu waliokufa
kwenye ajali kwa kipindi cha mwezi juni,
2016 ni 15 ikilinganishwa na mwezi mei,
2016 walikuwa 11, hivyo kuna ongezeko la
vifo vya watu wane sawa na asilimia 27%.
Katika kipindi hicho watu waliojeruhiwa
kwa kipindi cha mwezi juni, 2016 ni 21
ikilinganishwa na mwezi mei, 2016 ambapo
walijeruhiwa watu 06 hivyo kunaongezeko
la watu 15 sawa na asilimia 71.4% .
Katika kipindi cha mwezi juni, 2016 jumla
ya makosa 11,088 yalikamatwa na kutozwa
faini na kiasi cha tsh.329, 790,000
ikilinganishwa na mwezi mei 2016 ambapo
jumla ya makosa 10,389 ya ukiukwaji wa
sheria za usalama barabarani na
usafirishwaji yalitozwa faini sawa na tozo
ya shs. 311,670,000, hivyo kunaongezeko la
makosa 699 na ongezeko la maduhuri ya sh.
20,970,000 sawa na asilimia 6.3% jeshi la
polisi mkoa wa mwanza linaomba
ushirikiano kutoka kwa wananchi kwani
baadhi yao wanaendelea kuficha wahalifu
na uahlifu katika maeneo yao na kutokuwa
tayari kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi
kwa asilimia 100.
Chapisha Maoni