Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho
ataamua ni safu gani ambayo Wayne Rooney
atalichezea taifa lake ,kulingana na mkufunzi mpya
wa Uingereza Sam Allardyce.
Rooney mwenye umri wa miaka 30 alicheza safu
ya mashambulizi chini ya mkufunzi Roy Hodgson
katika michuano ya Euro 2016.
Lakini Allardyce amesema kuwa ni mapema mno
kuthibitisha iwapo Rooney,ambaye analiongoza
taifa lake katika ufungaji wa mabao atasalia kuwa
nahoda wa timu hiyo.
''Nadhani Wayne Rooney bado ana fursa kubwa
kuchezea Uingereza'', alisema mkufunzi huyo
mwenye umri wa miaka 61.
''Iwapo Jose atasema kwamba hatamchezesha
katika safu ya kati na anamchezesha katika eneo
la mashambulizi katika klabu ya Manchester
United,itakuwa haina maana yoyote mimi
kumchezsha katika safu ya kati''.
Posted Africa News Sports
Chapisha Maoni