0

Bara la Afrika litatunukiwa nafasi nyengine mbili
zaidi iwapo dimba la dunia litaongeza idadi ya
mataifa yanayoshiriki hadi 40 kuanzia mwaka 2026
kulingana na rais wa FIFA Gianni Infantino.
Infantino alipendekeza kuongezwa kwa timu hizo
kabla ya kuchaguliwa kwake na shirikisho hilo la
soka duniani.
Kwa sasa Afrika ina nafasi tano pekee katika
michuano hiyo .
''Pendekezo langu limekuwa timu 40 na iwapo hilo
litadhinishwa pendekezo langu ni kulipatia bara la
Afrika nafasi mbili zaidi'',alisema Infantino.
Hatahivyo hatua hiyo itaidhinishwa hadi mwaka
2026 huku timu 32 zikiwa tayari zimethibitishwa
kushiriki katika kombe la dunia la 2018 nchini
Urusi na 2022 nchini Qatar.



Posted Africa News Sports

Chapisha Maoni

 
Top