Kombe la Mataifa ya Afrika
mwakani, Gabon
wamemfukuza kocha wao
Jorge Costa ikiwa ni miezi
sita kabla ya kuanza kwa
michuano hiyo Januari.
Kocha huyo Mreno aliajiriwa
Julai 2014, na amefukuzwa
mara tu baada ya kupangwa
droo ya kufuzu Kombe la
Dunia mwaka 2018, Gabon
ikiwekwa kundi moja na Ivory
Coast, Mali na Morocco.
Costa alikuwa ndiye kocha
anayelipwa zaidi kuliko
wengine wote wanaofanya
kazi bara hiili kwa mujibu wa
taarifa za tovuti ya Gaboneco
mwezi Mei.
Kocha ghali zaidi barani
Afrika, Jorge Costa
amefukuzwa kazi Gabon
ikiwa ni miezi sita kabla ya
Fainali za Mataifa ya Afrika
"Kama ninapokea Euro
70,000 kwa mwezi, mshahara
ambao unaonifanya niwe
kocha anayelipwa vizuri zaidi
Afrika, ni kwa sababu mimi ni
kocha bora," alisema kocha
na mchezaji huyo wa zamani
wa Porto na Standard Liege,
Costa.
Alitoa maelezo hayo baada
ya maswali kuanza kuibuka
juu ya kiwango cha Gabon
uwanjani, hususan
wakifungwa 2-1 na
mabingwa wa Afrika, Ivory
Coast katika mchezo wa
kirafiki hivi karibuni.
Gabon, waliokuwa wenyeji
washirika wa Fainali za
Mataifa ya Afrika mwaka
2012 pamoja na Equatorial
Guinea, watakuwa wenyeji wa
fainali za 2017 kuanzia
Januari 21 hadi Februari 12.
Mrithi wa Costa anatarajiwa
kutajwa Julai 30 tayari kwa
mchezo wa kwanza wa
kufuzu Kombe la Dunia
mwezi Oktoba.
Chapisha Maoni