0
Maelfu ya raia wa Iceland wamekusanyika katikati
ya mji mkuu wa Reykjavik kukaribisha msafara wa
timu yao ya taifa kwa mafanikio iliyopata kwenye
michuano ya Kombe la mataifa Bingwa barani
ulaya mwaka huu 2016.
Wachezaji walipita katikati ya mji wakiwa ndani ya
basi kubwa la wazi wakisindikizwa na ngoma hadi
katika mlima wa Arnarholl ambapo mashabiki
waliwasalimia kwa shangwa na makofi .
Iceland ambayo imeshiriki kwa mara ya kwanza
mashindano makubwa ya Kombe la mataifa barani
Ulaya ilifikia ukingoni mwa mashindano mwaka
huu baada ya kupata kichapo kutoka kwa Ufaransa
kwa magoli 5 – 2.
Hata hivyo kabla ya kuondolewa ilionyesha
maajabu pale ilipoiondoa England kwenye hatua ya
kumi na sita bora.

Chapisha Maoni

 
Top