0
Kikosi cha Yanga kimeendelea na mazoezi kujiandaa na mechi ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Medeama ya Ghana.
Mazoezi ya Yanga kama ilivyokuwa jana,
yamefanyika kwenye Uwanja wa boko Veterani jijini Dar es Salaam chini ya Kocha Mkuu, Hans van der
Pluijm akisaidiwa na Juma Mwambusi na Juma
Pondamali.
Wakati wachezaji wengine wakiendelea kujifua,
Obey Chirwa natarajia kurejea nchini ndani ya siku
chache akitokea kwao Zambia.
Mmoja wa rafiki zake wa karibu, amesema matatizo
yaliyompeleka Zambia ameyafanyia kazi na
atarejea ndani ya siku chache.
“Hatakaa sana, kila kitu ameshughulikia. Ingawa ni
mambo mengi, atalazimika kuacha mengine
yashughulikiwe,” kilieleza chanzo.
Chirwa anarejea haraka ili kuendelea na na
maandalizi ya mechi ya Kombe la Shirikisho Kundi
A dhidi ya Medeama ya Ghana.
Mechi hiyo itapigwa Julai 15 kwenye Uwanja wa
Taifa jijini Dar es Salaam.

Chapisha Maoni

 
Top