0
Kocha Joseph Omog wa Simba, ameweka
msisitizo kwa kikosi chake kuanza mazoezi bila ya
kuwa na rundo la mashabiki.
Omog ambaye aliuambia uongozi angetaka
mazoezi yasiyo na mashabiki wengi ili wachezaji
wawe huru naye aweze kuwaona, amesisitiza hilo
tena.
Simba ilikuwa ianze mazoezi jana, lakini ikakosa
uwanja ambao ungeendana na anachotaka Omog.
"Kweli kocha anataka uwanja ambao atakuwa yeye
na wachezaji wake, anataka wawe huru, wacheze
wakijiachia na yeye apate nafasi ya kung'amua
anayotaka," alieleza mmoja wa viongozi wa Simba
walio katika kamati ya utendaji.
Pamoja na kuzuia mashabiki, Omog alizuia kikosi
chake kuanzia gym kama ilivyozoeleka, badala
yake akataka wachezaji kuanza na mazoezi ya
uwanjani na hasa kucheza mpira kwanza na
baadaye ataingia kwenye programu ya gym.
Raia huyo wa Cameroon aliyewahi kuipa Azam FC
ubingwa wa Ligi Kuu Bara mwala 2014, ndiye
kocha mpya wa Simba na atakuwa akisaidiwa na
Mganda, Jackson Mayanja.

Chapisha Maoni

 
Top