Mshambuliaji wa England na Tottenham, Harry Kane atasaini mkataba mpya kusalia White Hart Lane wenye thamani ya pauni milioni 5 kwa mwaka
wiki hii (Independent), Jose Mourinho ana uhakika
wa kumshawishi kiungo kutoka Ufaransa Paul
Pogba, 23, kurejea tena Manchester United miaka
minne baada ya kuondoka na kwenda Juventus
(Daily Mail), Manchester United wapo tayari
'kuvunja benki' ili kumsajili Pogba, huku dau
likidhaniwa kufika hadi pauni milioni 100
(Telegraph), kiungo wa Paris St-Germain, Blaise
Matuidi, 29, amepewa ruhusa ya kuondoka katika
kambi ya Euro 2016 ya Ufaransa na kwenda
England kwa ajili ya mazungumzo ya kuhamia
Manchester United (Goal), Manchester United na
Liverpool wote wanataka kumsajili kiungo wa Porto
Ruben Neves, 19 (Sun), Manchester City
wanakaribia kukamilisha usajili mwingine
unaodhaniwa kuwa wa pauni milioni 40 kumchukua
winga wa Schalke, Leroy Sane, 20 (Manchester
Evening News), Tottenham hatimaye wanakaribia
kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa AZ
Alkmaar, Vincent Janssen, 21, wiki hii na pia
wanataka kumsajili mshambuliaji wa Roma,
Antonio Sababria, 20 na Lucas Alario, 20 kutoka
River Plate (Daily Mirror), Arsenal wako tayari
kumpa Alvaro Morata, 23, mshahara wa pauni
144,000 kwa wiki kumshawishi kuhamia Emirates
(Don Balon), Crystal Palace wameongeza dau lao
kufikia pauni milioni 31.5 kumtaka mshambuliaji
wa Liverpool Christian Benteke, 25, baada ya dau
la pauni milioni 25 kukataliwa (Sun), Crystal Palace
wanakamilisha uhamisho wa beki wa West Ham
James Tomkins, 27 (Evening Standard), Chelsea
wanafikiria kutoa pauni milioni 12 kumchukua
mshambuliaji wa Southampton Graziano Pelle, 30,
iwapo watashindwa kumpata Morata kutoka Real
Madrid (Evening Standard), kiungo wa Liverpool
Lucas Leiva, 29, yuko tayari kuhamia Besitkas ya
Uturuki (Fanatik), Fernabahce wanataka kumsajili
mshambuliaji wa Newcastle Siem de Jong, 27
(Haberturk), West Ham na Crystal Palace ni
miongoni mwa timu za EPL ambazo Robin van
Persie, 32, ameruhusiwa kwenda na klabu yake ya
Fernabahce (Daily Mail), mshambuliaji wa zamani
wa Aston Villa Charles N'Zogbia, 29, anajaribu
kufufua mpira wake kwa kufanya mazoezi na
Sunderland (Birmingham Mail).
Chapisha Maoni